Semina ikiendelea.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Meneja
wa Usimamizi wa Mabenki ya
Huduma ndogo za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw.
Victor
Tarimo, akiwasilisha mada kuhusu "Usimamizi wa sekta ya fedha na maduka
ya kuendesha fedha za kigeni" kwenye semina ya waandishi wa habari za
uchumi na fedha jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja, akizungumza
wakati wa semina hiyo Machi 3, 2020.
NA K-VIS
BLOG/Khalfan Said, Arusha
SHERIA ya usimamizi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ya mwaka
1992 itafanyiwa mapitio baadaye mwaka huu na patakuwa na toleo jipya ili kuendana
na wakati, Meneja wa Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya
kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, amesema.
Bw. Tarimo amesema toleo la mwaka 2019 kuna mabadiliko kadhaa yalifanyika
na mojawapo ni kumeondolewa madaraja (Classes) ya maduka ya kubadilisha fedha
za kigeni.
Alisema wakati kwenye kanuni za mwaka 2017 kulikuwa na leseni daraja A na daraja B, ambapo leseni daraja
A waliruhusiwa kufanya miamala ya kubadilisha fedha za kigeni papo kwa hapo (Spot purchase ans sells of foreign currency)
tu, na leseni daraja B, waliruhusiwa kufanya miamala ya papo kwa hapo na
kufanya Money Transfer.
Hata hivyo Bw. Tarimo amesema kwenye kanuni za mwaka 2019 leseni za madaraja
haya ziliondolewa na imebaki daraja moja
tu na hii ilitokana na operesheni ya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni
mwaka 2019 mbapo BoT ilibaini kuwepo kwa udanganyifu ambapo mwenye leseni ya daraja
A alitoa huduma zote mbili za kufanya miamala ya papo kwa hapo (Spot purchase and sells of foreign
currency) na kufanya Money Transfer
kinyume na sheria.
Akifafanua zaidi amesema leseni ya daraja A ilimtaka mmiliki wa Bureau de change awe na mtaji wa kima
cha chini kabisa kiasi cha shilingi milioni 300 na daraja B bilioni 1, kwa
kanuni mpya ikaamuliwa kuwepo na leseni moja tu ambayo itamlazimu mtu anayetaka
kuanzisha biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kuwa shilingi bilioni 1 na
itaruhusu kufanya huduma zote mbili, yaani kuuza na kununua fedha za kigeni
lakini pia kusafirisha fedha za kigeni yaani Money Transfer.
No comments :
Post a Comment