Saturday, February 29, 2020

TANZANIA YAISHUKURU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA USHIRIKIANO WALIOTOA KUMUUNGA MKONO MKURUGENZI MKUU WA TMA KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA NAFASI YA MAKAMU WA TATU WA RAIS WA (WMO)



Kigali, Rwanda; Tarehe 08 Februari, 2020;
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Lawrence Kijazi amewashukuru wakuu wa Taasisi za Hali ya Hewa katika Jumuia ya Afrika Mashariki kwa
ushirikiano mkubwa waliompatia katika kuwania nafasi ya Makamu Watatu wa Rais wa WMO
“Naomba ushirikiano huu (teamwork) tulio uonyesha katika kipindi cha uchaguzi uendelee pia katika utekelezaji wa majukumu ya Kikanda kwenye uboreshaji na utoaji huduma za hali ya hewa”.Amesema Dkt. Agnes Lawrence Kijazi
Dkt. Kijazi amezungumza hayo wakati akitoa shukrani zake kwa niaba ya nchi katika Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Hali ya Hewa za Afrika Mashariki (Heads of EAC Meteorological Service Meeting), uliofanyika tarehe 7 hadi 8 Februari, 2020, jijini Kigali, Rwanda.
Dkt. Kijazi alisisitiza umuhimu wa kufanya vikaokazi vya pamoja ili kuhakikisha masuala muhimu yanayohusiana na utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kubadilishana taarifa za hali ya hewa yanapewa kipaombele.
“Kwa kutambua kuwa hali ya hewa haina mipaka ya nchi, hivyo ni wakati muafaka kwa Taasisi zetu kuwa na vikao vya kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha huduma, tukichukua mfano wa hali ya hatari iliyopo kwa sasa ya uvamizi wa nzige na mlipuko wa virusi vya corona ambapo kwa kiasi kikubwa hali hizo zinauhusiano na hali ya hewa”. Alisisitiza Dkt. Kijazi.

No comments :

Post a Comment