Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, apigwa marufuku kuingia Marekani.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani leo Ijumaa,
Januari 31 2020 marufuku hiyo pia inamhusisha mke wa Makonda Bi Mary
Felix Massenge.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Makonda anashutumiwa kwa kushiriki katika ukandamizaji wa haki za binadamu.
Ukandamizaji wa haki ambao Makonda anashutumiwa kuutenda ni pamoja na
kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na
usalama wa watu.
"Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu
huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa
kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na
sauti," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Michael Pompeo ametumia mtandao wake wa Twitter kutangaza marufuku hiyo.
No comments :
Post a Comment