Mkuu wa Kitendo cha
Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance Luhimbo
akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mikakati ya benki hiyo
katika kuendelea kuwasaidia wakulima katika uzalishaji bora, Hayo
ameyasema wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta
ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27-28
uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa
na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Afisa Masoko Tawi la NBC Samora,
Dustane Lipawaga (mwenye tisheti Nyekundu), akizungumza na baadhi ya
washiriki wa walipotembelea banda la NBC Tanzania wakati wa Mkutano wa
wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa
maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27na Feb 28 uliofanyika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara
ya Taifa NBC.
**************************
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC)
imesema kuwa itaendelea kushirikiana na kuwasaidia
wakulima hasa katika
kuwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali za kuboresha mazao yao kwa lengo la
kuhimarisha sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa wadau katika Kuongeza
tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda, Mkuu wa
Kitendo cha Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance
Luhimbo alisema benki hiyo imekuwa mbele kuwasaidia wakulima wadogo, wa
kati na wakubwa.
Alisema mikakati yao ya mbeleni
kwenye kilimo ni kuhakikisha wanaisaidia sekta hiyo kwa asilimia kubwa
na kwa kuanzia wameaandaa nyaraka inayoelezea ni kwa jinsi gani mtu
anaweza kumsaidia mkulima katika mazao yake na mtaji wake.
“Nyaraka hii imejikita katika
kilimo tu ambapo tunaangalia kwa njia gani tunaweza kumpatia huduma
nzuri mkulima na pia kuangalia tunaweza kumsapoti mkulima na kumpatia
ujuzi na utaalamu pamoja na kushirikana na Wizara katika mambo
mbalimbali.
Alisema mkakati huo wa kuwasaidia
wakulima ni endelevu hasa ukizingatia benki hiyo imekuwepo nchini kwa
miaka 52 sasa na wamekuwa wakiwasapoti wakulima hasa katika kuwapatia
mbinu mbalimbali za kilimo bora na chenye tija, kuwapatia ushauri juu ya
kuendesha shughuli zao za kifedha.”Tunaowataalamu wengi ambao
tunaendelea kuwatumia kuwasaidia wakulima lakini NBC tunashirikiana na
PASS ambao kazi yao kubwa kuwawekea ulinzi na usalama wa mazao kwa
wakulima,” alisema
Evance Luhimbo alimalizia kwa
kusema mtu akimsapoti mkulima atakuwa ameweza pia kusapoti masuala ya
viwanda ambayo ndio ajenda kubwa nchini.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo,
Hussein Bashe alisema ili kufikia uchumi wa kati katika sekta ya
Viwanda, mahitaji ya wakulima, wavuvi na wafugaji hayawezi kutekelezwa
kwa bajeti ya serikali pekee bali wadau wakubwa wajitokeze kuwekeza.
Bashe aliseema katika sekta ya
Kilimo kumekuwa na changamoto kubwa ya bajeti, kwani haiwezi kutosheleza
kwenye kuleta maendeleo ya kilimo na kufikia malengo yaliyowekwa na
serikali.
Kuhusu National Bank of Commerce (NBC)
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki hii inaanzia mwaka 1967
ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha,
zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka
sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa
ya biashara, iligawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding
Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka
2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55%
kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania
ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama
mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za
benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.
Benki ya NBC ni benki pekee ya
kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5
na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali
za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali.
Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.
Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us NBC_Marke8ngDepartment@nbc.co.tz
No comments :
Post a Comment