*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Mvua zinazoendelea kunyesha katika
maeneo mbalimbali nchini zimesababisha kufuriko kwa
mito mikubwa ya
Mkondoa na kuleta uharibifu katika njia za reli.
Akizungumza na wanahabari Jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Reli Tanzania TRC, Masanja
Kadogosa amesema kuwa katika maeneo ambayo yameharibiwa na mvua Kilosa
(Mororgoro), Gulwe (Mpwapwa),Igandu, Zuzu na Makutupora (Singida).
“Takribani maeneo 26 yameathirika
kati ya hayo 10 yako katika hali mbaya ambapo tuta la reli na baadhi ya
makalavati yamezolewa na maji”. Amesema Kadogosa.
Aidha Kadogosa amesema kuwa
kutokana na hali hiyo wahandisi wa TRC wako katika maeneo mbalimbali
yaliyoharibika kufanya tathimini halisi ya gharama za miundombinu ya
reli iliyoathirika matengenezo ya muda mfupi yanayoendelea katika maeneo
ambayo maji yanapungua ili kurejesha huduma za usafiri wa treni za
abiria na mizigo ambapo hadi sasa maeneo ya kati ya Dodoma na Makutupora
yamerekebishwa.
Uharibifu huo umesababisha
kusimama kwa huduma ya usafiri kwa njia ya reli inayotoka Dar es Salaam
hadi Kigoma, Mwanza na Mpanda mpaka ukarabati utakapokamilika.
No comments :
Post a Comment