Kiongozi wa kanisa la Inuka Uangaze,
Nabii na mtume Boniface Mwamposa amelazimika kusitisha ibada kwa ajili
ya kuitikia wito wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Tanzania kulikotokea
vifo vya waamini wake.
Mwamposa ambaye huendesha ibada zake
katika eneo la Tanganyika Packers, leo Jumapili Februari 2, 2020,
amelazimika kufupisha ibada ya kwanza na kuanza safari ya kuelekea Moshi
alikoitwa na polisi.
Kawaida ibada hiyo huisha kati ya saa saba hadi saa nane mchana, lakini leo imeisha saa 4:30.
Mwamposa akiwa ameambatana na wasaidizi wake, aliondoka katika eneo hilo la Kanisa 4:30 leo asubuhi.

No comments :
Post a Comment