Mbunge wa Viti Maalumu, Bupe
Mwakang’ata (CCM), Mkoa wa Rukwa, akiuliza swali kwa Waziri wa Maji
bungeni Dodoma kwamba Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga visima
virefu vya maji katika Wilaya ya Nkasi ili kutatua changamoto ya maji
iliyopo
………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Bupe
Mwakang’ata,amehoji Serikali ina mpango gani wa
kujenga visima virefu
vya maji katika wilaya ya Nkasi ili kutatua changamoto ya maji iliyopo.
Akiuliza swali bungeni
leo,Mhe.Bupe amesema ”Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga visima
virefu vya maji katika Wilaya ya Nkasi ili kutatua changamoto ya maji
iliyopo”amehoji
Akijibu swali hilo Naibu Waziri
wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa kwa kutambua tatizo la maji lililopo
katika Wilaya ya Nkasi Serikali katika mwaka wa fedha 2019/2020 imepanga
kuchimba visima virefu 9 katika maeneo ya Masolo, Katogolo, Mpata,
Mienge, Itindi, Kacheche, Lyele, Mbwendi na Kakoma.
Aidha Aweso amesema kuwa kiasi cha Shilingi Milioni 315 kimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kazi hiyo.
“ Hadi kufikia mwezi Disemba 2019,
Visima 7 vimechimbwa katika vijiji vya Masolo, Katogolo, Mpata, Mienge,
Kanazi na Ipanda na kiasi cha Shilingi Milioni 220 kimetumika katika
upimaji na uchimbaji wa visima hivyo ambavyo vitatumika kama vyanzo vya
maji katika vijiji husika”amesema Mhe.Aweso
Hata hivyo amesema kuwa katika
mpango wa muda mrefu wa kutatua tatizo la maji katika Wilaya ya Nkasi,
katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imepanga kutumia zaidi ya
Shilingi Bilioni 1.3 kwa kupitia Programu ya PforR kwa ajili ya
kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Nkasi.
“Wizara imeshatuma fedha hizo kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji 6 Wilayani Nkasi ambapo miradi
yote hiyo itatekelezwa kwa mfumo wa Wataalam wa ndani (Force
Account)”amesisitiza
No comments :
Post a Comment