Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi amemsimamisha
kazi ofisa ardhi wa Wilaya ya... Kigamboni ambaye siku kadhaa zilizopita
Rais Magufuli alitaka achukuliwe hatua kwa kuwa ni mtoro
Siku
hiyo Magufuli alisema, “Nina tatizo na ofisa ardhi wa Kigamboni ni
mtoro na hajafanya kazi karibu miezi mitatu, aliandikiwa barua na Wizara
ya Ardhi ili ashughulikiwe ila bado wizara wanaleta mshahara wake.
Najua wizara watafikishiwa ujumbe, kama ni mtoro atoroke kabisa,
sifahamu mkurugenzi mmechukua hatua gani kwa ofisa ardhi huyo ambaye
hafanyi kazi.”
Katika
maelezo yake ya jana wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa
ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, Lukuvi alisema mtumishi
huyo amesimamishwa kazi.
"Bahati
nzuri tulishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni na
tumeshamsimamisha kazi wakati hatua za kinidhamu zikiendelea .Kama
kutakuwa na uhitaji tutaleta mtu mwingine," alisema Lukuvi.
No comments :
Post a Comment