Mkuu
wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Nakonde, Mhe. Field Simwinga (kulia) wakipongezana baada ya Uzinduzi
Wa Utekelezaji Wa Makubaliano Ya Mpango Wa Urasimishaji Wa Matumizi Ya
Kwacha Na Shilingi. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tawi la
Benki Kuu ya Tanzania Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi na Mkurugenzi wa huduma za Kibenki na Mifumo ya Malipo Benki Kuu ya Zambia, Bw. Lazarous Kamanga(wa kwanza kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma
Irando akizungumza wakati wa Uzinduzi Wa Utekelezaji Wa Makubaliano Ya
Mpango Wa Urasimishaji Wa Matumizi Ya Kwacha Na Shilingi.
Kikundi cha maigizo kutoka Zambia kikitoa burudani kwa wananchi waliohudhuria tukio hilo
Mkuu
wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Nakonde, Mhe. Field Simwinga (kulia) wakifungua kitambaa kuashiria Uzinduzi
Wa Utekelezaji Wa Makubaliano Ya Mpango Wa Urasimishaji Wa Matumizi Ya
Kwacha Na Shilingi. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tawi la
Benki Kuu ya Tanzania Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi na Mkurugenzi wa huduma za Kibenki na Mifumo ya Malipo Benki Kuu ya Zambia, Bw. Lazarous Kamanga(wa kwanza kulia)
Kutokea kushoto ni Mkurugenzi
wa Tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi , Mkuu wa
Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando, Mkuu wa Wilaya ya Nakonde, Mhe. Field
Simwinga na Mkurugenzi wa huduma za Kibenki na Mifumo ya Malipo Benki
Kuu ya Zambia, Bw. Lazarous Kamanga.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi akizungumza wakati wa Uzinduzi Wa Utekelezaji Wa Makubaliano Ya Mpango Wa Urasimishaji Wa Matumizi Ya Kwacha Na Shilingi.
…………………………………………………………………………………………………………
Benki Kuu ya Tanzania na Benki Kuu
ya Zambia zimerasimisha matumizi ya Kwacha ya Zambia na shilingi ya
Tanzania kwenye mpaka wa Tunduma na Nakonde ambapo wananchi wataweza
kutumia fedha za nchi hizo mbili katika shughuli zao za kila siku za
kiuchumi bila
kubadilisha.
Akizungumza kwenye hafla hio
iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nakonde, Mhe. Field Simwinga pamoja
na Viongozi wa Serikali na Wakuu wa Taasisi mbalimbali kutoka Zambia na
Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando alieleza kuwa
Urasimishaji wa Matumizi ya Kwacha na Shilingi utaongeza nguvu katika
jitihada mbalimbali zilizokwishafanyika ili kuongeza chachu ya biashara
katika eneo la mpaka wa Tunduma na Nakonde.
“Utaratibu huu utaondoa mlundikano
wa Kwacha upande wa Tanzania. Kama mnavyojua, Wananchi wa Zambia
wananunua bidhaa na huduma kwa wingi kutoka Tunduma kwa kutumia Kwacha
wakati Watanzania hawawezi kununua vitu kutoka upande wa Zambia
(Nakonde) kwa kutumia Shilingi. Kwa sababu hiyo kunakuwa na Kwacha
nyingi upande wa Tanzania ambazo hatimaye zinaishia mikononi mwa wauzaji
wasio rasmi”
Urasimishaji huo unategemewa
kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kuwaondolea wananchi gharama za
kubadili fedha kwani kuanzia sasa watauza na kununua kwa kutumia Kwacha
na Shilingi kwa pamoja.
“Ushiriki wa Benki zetu hapa
Mpakani katika kununua na kuuza Kwacha na Shilingi kunawapatia wananchi
huduma salama za ubadilishaji wa fedha, ambapo wataepusha hatari ya
Wananchi kupewa fedha bandia. Pia benki zitatoa viwango sahihi vya
ubadilishanaji wa Kwacha na Shilingi hivyo kulinda thamani ya fedha
zetu”, aliongeza.
Mhe. Irando alisema kuwa tukio
hilo litaimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Serikali ya Zambia
na Tanzania na kuboresha hali ya maisha ya wananchi kwa kurahisisha
shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Uzinduzi wa utaratibu huo ni
utekelezaji wa Hati ya Makubaliano (MOU) iliyosainiwa tarehe 21 Septemba
2018, kama jitihada za serikali ya Zambia na Tanzania za kumaliza
changamoto ya muda mrefu ya biashara holela ya fedha za kigeni katika
mpaka wa Tunduma na Nakonde.
No comments :
Post a Comment