Mkurugenzi wa Maktaba kuu Sichana
Haji Foum akitoa hotuba ya makaribisho katika hafla ya Uzinduzi wa Klabu
ya kusoma Vitabu katika Ukumbi wa Maktaba kuu Mpirani Akrotanal mjini
Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bakiza Dk Mohamed
Seif Khatib akizungumza machache katika hafla ya Uzinduzi wa Klabu ya
kusoma Vitabu katika Ukumbi wa Maktaba kuu Mpirani Akrotanal mjini
Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Riziki Pembe Juma akitoa hotuba ya uzinduzi wa Klabu ya kusoma
Vitabu iliofanyika katika Ukumbi wa Maktaba kuu Mpirani Akrotanal
mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Riziki Pembe Juma akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya
uzinduzi wa Klabu ya kusoma Vitabu iliofanyika katika Ukumbi wa
Maktaba kuu Mpirani Akrotanal mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Klabu ya kusoma
Vitabu Bimaryam Hamdani akitoa hotuba na kumkaribisha mgeni Rasmi
katika hafla ya Uzinduzi wa Klabu ya kusoma Vitabu katika Ukumbi wa
Maktaba kuu Mpirani Akrotanal mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
**************************
Na Khadija Khamis –Maelezo- Zanzibar 01/02/2020.
Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma amewataka wanafunzi wa skuli mbali
mbali za Zanzibar pamoja na jamii kiujumla kuitumia Maktaba Kuu ya
Zanzibar kwa
lengo la kujiongezea uwelewa pamoja na ufahamu wa mambo
mbali mbali ikiwemo historia ya nchi .
Hayo aliyasema
huko katika Ukumbi wa Maktaba kuu Maisara wakati wa Uzinduzi wa Klabu ya
kusomea vitabu yenye lengo la kuihamasisha jamii kupendelea kusoma
vitabu.
Amesema kufanya
hivyo kutasaidia kujiongezea taaluma na kuirejesha hadhi ya awali
iliyopotea ya utamaduni wa kusoma vitabu kwa kuimarisha lugha ya
Kiswahili na nyenginezo za kigeni .
Aliwataka
wananchi kujiunga na Klabu hiyo ili kuongeza uwelewa wa mambo tofauti
ikiwemo mambo ya kihistoria, utamaduni,kisiasa,kiuchumi, kiufundi,
kilimo na mengine mengi .
“Waliyafanya
waliyaandika tunayasoma na kuyajuwa na kuridhisha vizazi vijavyo kama
vile Mapinduzi ya Zanzibar wengi tulikuwa hatujazaliwa lakini tumesoma
vitabu tumejuwa hii ndio hazina moja kubwa sana “, alisema Waziri wa
Elimu
Aidha alisema
ushajihishaji wa kujisomea vitabu kwa wanafunzi kutawasaidia katika
mitihani yao na wataachana na simu ambazo hawazitumii ipasavyo jambo
ambalo linazorotesha maendeleo yao ya kielimu .
Alifahamisha kuwa
kuna vitabu vingi vizuri vya zamani ambavyo wanafunzi hawavijui kama
vile Alfu ulela ulela,Mzimu wa watu wa kale na vyengine vingi iko haja
kuvisoma na kuvielewa dhamira ya mtunzi aliyoikusudia ambayo ina ujumbe
kwa jamii na vizazi vijavyo kupitia tahakiki mbali mbali zinazofanywa na
wataalamu wa klabu hiyo .
Hata hivyo Waziri
huyo alitoa rai kwa jamii kutumia wigo za tamaduni za kigeni za kubeba
vitabu na kuvisoma katika safari zao kama vile katika ndege na safari za
masafa marefu .
.
Nae Mwenyekiti wa
Bakiza Dkt. Mohamed Seif Khatib alisema zamani maktaba iliitwa jengo la
wajinga kwa maana ya kwamba ukitaka upunguze ujinga ufike kujisomea
vitabu mbali mbali uweze kupata uwelewa mpana wa mambo .
Alisema elimu
nzuri ya kujiimarisha ni kununua vitabu mbali mbali kwa kuweka maktaba
majumbani kufanya hivyo kutasaidia wanafunzi kujisomea vitabu hivyo .
Aliwafahamisha
wanafunzi kuwa na muamko wa kusoma vitabu na kuvielewa sio kuhifadhi
uhakiki jambo ambalo linasababisha kushindwa kuingiza mawazo yao
katika kujibu mitihani.
“wanafunzi
wanakunywa uhakiki mwanzo mwisho wakati wa mitihani wanacheuka vile vile
hii haipendezi kwasababu wanatakiwa waingize mawazo yao kwa mujibu
walivyokisoma kitabu hicho”, alisema Dkt Mohamed.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bi Mariamu Hamdani alisema kuwa tabia ya
kusoma vitabu inaadhiri kutoweza kuiacha pindipo ukiizowea na hukufanya
uwe na uwelewa mpana wa kujuwa mambo mengi kupitia usomaji wako wa
vitabu mbalimbali .
Alifahamisha
Clabu hii itafanya uhakiki wa vitabu mbali mbali kwa kuanzia na kitabu
cha Bwana Msa, “Mzimu wa watu wa kale” lengo ni kuihamasisha jamii
kutaka kuufahamu mzimu huu umefanya nini kupitia maktaba za vitabu
hivyo
Alifahamisha
wataendelea kuhakiki vitabu kupitia klabu hiyo ili kuwawezesha wanafunzi
na jamii kuvifahamu vitabu hivyo kwa ufasaha na kujuwa dhamara ya
Mtunzi kwa jamii katika harakati ya kutoa elimu kupitia fasihi andishi .
Klabu ya kusoma
vitabu imeanzishwa Oktoba mwaka jana ikiongozwa na Mwenyekiti wa Klabu
hiyo Bi Mariam Hamdan na Katibu Dkt Mwanahija Ali Juma .
No comments :
Post a Comment