Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Ludovick
Nduhiye wakiwa katiza picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Sekretarieti ya
COMESA ulioongozwa na Balozi Dr. Kipyego Cheluget.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Katibu
mkuu anayeshughulikia miradi kutoka sekretarieti ya (COMESA) Balozi Dr.
Kipyego Cheluget.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe akiongoza kikao kujadili utekelezaji wa
mradi wa uwezeshaji biashara (Trade Facilitation) na kuimarisha biashara
ya mipakani (Cross Border Trade).
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe akisisitiza jambo kwa na Balozi Dr.
Kipyego Cheluget ambaye ni Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia miradi
kutoka sekretarieti ya (COMESA) kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Biashara Ndugu Ludovick Nduhiye katika ofisi za wizara
Mtumba, jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 27 Februari, 2020 amepokea
ujumbe kutoka Sekretarieti ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa
Afrika (COMESA) ulioongozwa na Balozi Dr.Kipyego Cheluget, ambaye ni
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miradi.
Ujumbe huo ulifika katika ofisi za
wizara zilizopo katika eneo la Mtumba jijini Dodoma lengo likiwa ni
kukutana na Menejimenti ya Wizara kuzungumzia utekelezaji wa mradi
unaohusu uwezeshaji biashara (Trade Facilitation) na kuimarisha biashara
ya mipakani (Cross Border Trade).
Pande zote mbili zimekubaliana
kushirikiana kwa karibu zaidi katika utekelezaji wa mradi huo ambao
unatarajia kuchochea na kurahisisha biashara kwa nchi wanachama wa
Jumuiya za COMESA, EAC na SADC.
No comments :
Post a Comment