Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akipokelewa na Naibu Katibu
Mkuu Bw.Ludovick Nduhiye mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara
hiyo Mtumba jijini Dodoma akichukua nafasi ya Katibu Mkuu aliyemaliza
muda wake Prof. Joseph Buchweishaija.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akisalimiana na na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya sera na mipango Bw.Alfred Mapunda mara baada ya
kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma akichukua
nafasi ya Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Prof. Joseph Buchweishaija.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akisalimiana na na Mkurugenzi
wa idara ya viwanda vidogo na biashara ndogo Dk.Consolatha Ishebabi mara
baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma
akichukua nafasi ya Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Prof. Joseph
Buchweishaija.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akisalimiana na na Mkurugenzi
wa idara ya biashara ,Ally Gugu mara baada ya kuwasili katika ofisi za
wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma akichukua nafasi ya Katibu Mkuu
aliyemaliza muda wake Prof. Joseph Buchweishaija.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akisalimiana na na Mkuu wa
kitengo cha habari Bi.Mindi Kasiga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma akichukua nafasi ya Katibu Mkuu
aliyemaliza muda wake Prof. Joseph Buchweishaija.
Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake
Prof. Joseph Buchweishaija (kushoto) akikabidhi ofisi kwa Katibu Mkuu
Mpya Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,mara baada ya
kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akizungumza na wafanyakazi wa
wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba
jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe.Innocent Bashungwa,akimkaribisha Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,mara baada ya kuwasili katika
ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,akimkaribisha Katibu Mkuu Mpya Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Mpya Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi za
wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe.Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu
Mpya Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe,mara baada ya
kuwasili katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Katibu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka wafanyakazi wa
Wizara hiyo
kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuyafikia matarajio ya Mhe. Rais
John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
Viwanda.
Akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu
alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Prof. Shemdoe alimshukuru Mhe Rais kwa
kumuamini na kumteua na kumuona anafaa kuongoza Wizara hiyo pia
aliwataka watumishi kumpa ushirikiano wa kutosha.
“Hii ni wizara iliyojenga ajenda ya serikali ya awamu ya tano
hivyo tuje sisi tumepewa kazi kubwa ambayo tunapaswa kufanywa ili wizara
hii itoe matokeo yanayotarajiwa na Mhe. Rais Magufuli.
“Nawahakikishia kuwapa ushirikiano na wakati wote ofisi yangu
itakuwa wazi bila kikwazo chochote muda wote nitapatikana
nitakapohitajika.
Akielezea matarajio yake kwa watumishi hao Prof. Shemdoe
aliwataka kusimamia ajenda ya Tanzania ya Viwanda na pia anatarajia kuwa
watafanya kazi kwa uharaka na ufanisi.
Naye Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Prof. Joseph Buchweishaija alimpongeza kwa kuteuliwa kuongoza Wizara hiyo.
“Nampongeza Prof kwa kuteuliwa kuongoza Wizara hii, hii ni
wizara yenye watu wanaojituma na kufanya kazi kuanzia uongozi wa juu
hadi wafanyakazi”.
Akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Bw. Ludovick Nduhiye
alieleza kuwa lengo la kikao hicho ni kufahamiana na kutambuana na
alihaidi kufanyika kwa kikao kingine cha kutambuana zaidi.
Mwenyekiti wa TUGHE, Wizara ya Viwanda alielezea kuhusu umuhimu wa baraza la wafanyakazi katika kupitisha bajeti ya Wizara
“Ulidokeza kuhusiana na maandalizi ya bajeti Wizara, Tunatakiwa
kupata wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, tunarajia mwezi huu wa pili
kamishna wa kazi atakuja kutafanya uchaguzi ili baade baraza hilo liweze
kupitisha bajeti ya Wizara kama ilivyo utaratibu”.
No comments :
Post a Comment