Friday, February 28, 2020

GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) PROFESA LUOGA ASISITIZA USAFI MATUMIZI YA NOTI



Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa BoT leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia Noti safi. kulia ni Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) na katikati ni Dkt. Bernard Y. Kibesse Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa BoT leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia Noti safi kushoto ni  Bw. Julian Banzi Raphael Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani
………………………………………
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Florens Luoga amesema benki zote zinapashwa kurudisha pesa zote chafu benki kuu ya Tanzania ili ziharibiwe na kuingizwa pesa Safi kwenye
mzunguko huku akiwaonya wananchi wanaotumia pesa kinyume na utaratibu ikiwemo kuziandika maandishi kuwa ni kosa la jinai na watakamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Akitoa Rai hiyo mbele ya waandishi wa habari habari Gavana wa benki kuu ya Tanzania Florens Luoga amesema Hadi Sasa benki kuu haijachapisha Wala kuingiza pesa mpya kwenye mzunguko Tangu mwaka 2009 na kwamba pesa iliyopo kwenye mzunguko inatosha kabisa kwa mahitaji ya soko.
Benki kuu ya Tanzania inatangaza Vita kwa watengenezaji wasaambazaji na watumiaji wa Noti bandia huku ikipanga kuanzisha mkakati maalum wa kuwafundisha wananchi namna ya kufanya utambuzi wa Noti halali ili kuepukana na utapeli.
Aidha amesema benki kuu itaendelea kutekeleza Sera yake ya Sarafu Safi huku akiziomba benki zote kuhakikisha zinatoa huduma rafiki kwa wananchi ili waweze kutumia mifumo rasmi na kwamba ndani ya saa 24 mteja anatakiwa kupatiwa ufumbuzi wa matatizo ya kifedha endapo imetokea ikiwa ni dhumuni la kuongeza haki katika huduma za kibenki.

No comments :

Post a Comment