Tuesday, February 4, 2020

Fahamu haki ya pensheni yako baada ya talaka

Pension warning: People getting a divorce in pictures
Sheria ya talaka inapaswa kurekebishwa ili haki ya pensheni ya talaka itolewe sawa kwa waliotalakiana, mfano rasilimali iliyochumwa, pamoja kama ilivyo kwa haki ya pensheni ya urithi wakati mmoja wa wanandoa anapofiwa na mwenza wake.

Na Christian Gaya,
majira 31.Januari.2020
Michango ya pensheni ya hifadhi ya jamii kisheria ni rasilimali za pamoja zilizochumwa wakati wa ndoa inayotambulika kisheria. Michango ya pensheni ya hifadhi ya jamii ni vitega uchumi vya
pamoja vilivyoweka kwa mategemeo ya siku za baadaye ya kwamba wanandoa wote watakuja kunufaika nayo baada kufikisha umri wa hiari au wa lazima wa kustaafu.
Lakini kutokana na sababu mbalimbali unaweza ukakuta ya kuwa kati ya ndoa 10 zilizokuwa zimefungwa kisheria na kimila ndoa 5 zilisha vunjika kabla ya kufikia miaka 30 ya kusherekea ndoa baada ya kuoana.
Talaka zinaweka alama ya kudumu ya mwisho wa mali na vitega uchumi vyenu mlivyokuwa mmewekeza pamoja katika maisha ya ndoa yenu ya maisha, ndiyo mwisho wa uwezo wenu kifedha na vitu vya kugawana mbele ya safari ya maisha.
Mwongezeko wa hizi talaka imekuwa ndiyo chanzo cha madadiliko ya sera za umma na marekebisho ya sheria ya maisha ya familia yanayohusiana na usuruhishi na kuvunjwa kwa ndoa mara kwa mara.
Sera za umma zinazoshughulika na ndoa za watu binafsi zinahusiana na talaka zikiwepo na jinsi ya mgawanyo wa mali zilizochumwa pamoja wakati wa ndoa yenu zina umuhimu mkubwa kujumuishwa kwa ajili ya kupunguza hali hatarishi za majanga yanayoweza kutokea kwa sasa na kwa baadaye kwenye maisha ya wana ndoa.
Siyo hivyo tu sera hizo ni pamoja ya kuhakikisha ya kuwa zinahamasisha kutendeka kwa kutokea haki ya ukweli kati ya wanatalaka waliopata maumivu ya kuvunjika kwa ndoa yao, yanapunguza msongo wa mawazo na hata pia yanapunguza gharama za kushughulikia talaka.
Ambapo kwa mifuko hii ya hifadhi ya jamii Tanzania hakuna hata mmojawapo ambao umeweka sheria kama hii ya juu ya mgawanyo sawa wa idadi ya michango ya pensheni pale inapotokea ya kuwa wanandoa hawa wametengana au wamepeana talaka.
Ingawa mapato ya idadi ya michango ya pensheni yanaweza kuwa tofauti, kwa sababu ya tofauti ya kazi na tofauti za kimapato. Idadi kubwa ya wanawake ni rahisi sana kupata wastani wa mapato pungufu kwa sababu ya kupata kazi za muda mfupi.
Hii inajumuisha pamoja na kazi ambazo zina viwango vya chini na tabia ya kuajiri na kupungufu mara kwa mara kwa sababu ya hali ya uchumi wa nchi. Hata kama watakuwa wameajiriwa, wanawake waliolewa siyo rahisi wastani wa mapato yao kufanana wenza wenzao walioajiriwa, pamoja na kupunguza ufume dume.
Kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha ya kuwa sheria hii inarekebishwa ya kuhakikisha ya kuwa haki ya pensheni ya talaka inatendewa sawa kwa wana talaka wote kama rasilimali iliyochumwa kwa pamoja kama ilivyo kwenye haki ya pensheni ya urithi pale mmojawapo wa wanandoa anapofiwa na mwenza.
Pensheni ilyochumwa wakati wa ndoa kwa jumla inachukuliwa kuwa mali ya pamoja ya wanandoa wote yaani mme na mke. Hii ina maana ya kwamba hata mmojawapo ambaye alikuwa siyo mfanyakazi mwajiriwa kwa kumwezesha yeye kuchangia katika mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii anakuwa na haki ya kunufaika na hiyo pensheni ya mwenza aliyekuwa naye wakati anachangia na kuishi pamoja kwa hali na mali.
Mfano chukulia ya kuwa mwanamke alikuwa mama wa nyumbani. Ina maana alikuwa na mchango mkubwa wakati wowote wa kulea watoto pamoja na baba yao wakati akiwa nyumbani na baada ya kutoka nyumbani alipatiwa huduma zote za lazima kutoka kwa mama wa nyumbani.
Pia ni kwamba alimwezesha mme wake kuwa na amani moyoni wakati wowote akiwa kazini, alimwezesha mme wake hata kuongezeka kwa ufanisi kazini wake wa kufanya kazi kwa bidii akiwa kazini. Na huenda hata kuthibitishwa na kupandishwa ngazi za mshahara mmoja wapo kila mmoja huwa anakuwa na mchango wake wa mafanikio. 
Hata hivyo, ni juu ya mahakama ya talaka kuamua hali halisi ya jinsi mali kutokana na pensheni ni inavyowezwa kugawanywa baada ya kutegengana kisheria, na kama wote wakiwa waathirika faida ni kulipwa na kugawana sawa au hapana.
Kwa nchi zilizoendelea kesi kama hizi za juu ya kugawana pensheni ya mme au mke baada ya kutengana ni kitu cha kawaida kama kesi zingine za kutalakana.
Ingawa kwa nchi za Kiafrika kama Tanzania jambo kama hili haliwekewi maana kabisa huenda ni kwa sababu ya kukosa elimu ya haki ya pensheni na hali ya kuwepo kwa mfumo dume ya kuona ya kuwa mwanamke ni kama chombo cha kutumiwa tu.
Na ndiyo maana kuna sheria na mila na desturi za Kiafrika ambazo zinasema mwanamke hana hata haki ya kumiliki ardhi na hivyo hata kwenye mirathi ya familia au ukoo kutohusishwa kwa migao kama hiyo ya kumiliki ardhi.
Na hata kwenye sheria za hifadhi ya jamii jambo hili la haki ya pensheni baada ya wenza hawa kutengana, mwanamke au mwanamme kupata sehemu yake halijagusiwa hata kidogo wala kuongelewa, ingawa wameweza kugusia juu ya haki ya pensheni mirathi baada ya mme au mke kuaga dunia.
Na kwamba pensheni hiyo inasimamishwa iwapo mme au mke mfiwa atangundulika ya kuwa ameolewa au ameowa tena, kwa sababu atakuwa amempata kumpatia mkate wa kila siku wa kumwezesha kuishi.
Hivyo basi hata kwa upande wa talaka amri ya mahakama ni muhimu sana kwa mtu ambaye amepata na janga kama hili la talaka naye kupata sehemu ya pensheni yake kama mmojawapo wa mwenza mwenzake alikuwa mwanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii.
Kwa sababu tumeona mara nyingi kwa wanandoa wengi wanapopeana talaka kutotilia maanani jambo hili hata kidogo wakati ni jambo la muhimu ingawa sheria nayo iko kimya. Ambapo huenda inaweza kuwa kwa sababu ya kutojua sheria au kwa sababu ya aina ya mfumo wa maisha tuliorithi.

No comments :

Post a Comment