…………………………………………………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
MKUU Wa Wilaya Ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa
ameiagiza halmashauri ya Bagamoyo kutumikia wananchi kwa maslahi mapana
ya jamii pamoja na kusimamia chanzo kikuu cha machimbo ya mchanga
ambacho kinalegalega na kusababisha kushuka kwa mapato.
Aidha mkuu huyo wa
wilaya, ameelekeza kupatiwa maelezo ya kina ni kwanini mashine za
makusanyo (posi) zinazimwa na kushindwa kukusanya mapato kwa muda mrefu
na hivyo kuhitaji maelezo ofisini kwake.
Akizungumza na
watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo, Zainab alisema , wabadilike
,wasimamie na kufuatilia mapato pasipo kujenga uongo na udanganyifu kwa
maslahi ya matumbo yao.
“Haiwezekani mapato
ya mchanga yanashuka ,licha ya vyombo vya ulinzi na usalama kubaini
mianya na udanganyifu, hasa katika eneo hili la mchanga, mmefikia hatua
ya kuidanganya hadi TAKUKURU mnapotosha taarifa na takwimu sahihi za
makusanyo ili kujinufaisha””
“Ninahitaji maelezo
pia kwanini mnazima posi ,hizi mashine mnazima kwa kipi?!nahitaji
maelezo na nakala nyingine ielekezwe kwa mkuu wa mkoa na nyingine
TAMISEMI”alisema Zainab.
Zainab alieleza,
kuzimwa kwa posi ni kukiukwa maelekezo ya TAMISEMI ,halmashauri ni eneo
lenye heshima na hadhi yake,ambapo inapaswa kuendeshwa kwa kuzingatia
sheria,kanuni na taratibu hivyo pasifanyiwe mchezo ama kuendeshwa
kiholela (kihuni).
Nae mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Ally Ally Issa alisema , hali ya mapato hairidhishi
kutokana na chanzo mama cha mchanga kuyumba ambapo makusanyo yamefikia
asilimia 43 wakati walitakiwa kufikia asilimia 50 kwa kipindi hiki cha
miezi sita.
Alifafanua kwamba,
kutokana na hilo wamebaini machimbo holela ya mchanga 23 na sasa wapo
katika mkakati wa kuyafunga baadhi ya machimbo na mengine kuyarasimisha
na kuongeza usimamizi ili kunusuru utoroshaji na kuongeza mapato.
Alieleza kwamba, machimbo ambayo yamesharasimishwa ni pamoja na Nzole,Fukayose na Mapinga.
Kuhusu posi ,Ally
alieleza tatizo kubwa kuna nyingine zimeharibika na nyingine
hazifanyikazi hivyo pia wamenunua posi mpya 43 ili kupunguza changamoto
iliyojitokeza.
Kwa upande wake ofisa mazingira Bagamoyo, Cleophace Murugwa aliwataka wachimbaji kufuata taratibu za kupata kibali na leseni .
Alibainisha ,kwasasa
wanapambana na wale wanaofanya uchimbaji wa maeneo yasio rasmi, na
atakaeenda kinyume na taratibu sheria inachukua nafasi yake.
Murugwa alitaja maeneo yaliyo rasmi ni Kilomo eneo la Buma, Yombo -Chasimba na Fukayose huko Mwavi.
No comments :
Post a Comment