Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo (kulia) na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Justice Kijazi wakipanda miti katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti yaliyofanyika kiwilaya Kijiji cha Nkhoiree Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja jana.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo (kulia)
na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Justice Kijazi wakizungumza na Wanafunzi
wa Shule ya Msingi ya Nkhoiree kabla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Justice Kijazi, akizungumza
Msafara wa kwenda kupanda miti.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo, akizungumza.
Miti ikipandwa.
Mkutano wa uzinduzi ukifanyika.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU
wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Edward Mpogolo amepiga marufuku
uchomaji wa mkaa na uvunaji wa mbao katika wilaya hiyo bila kufuata
taratibu za uvunaji wa miti kama GN No. 417 ya Mwaka 2019 inavyo
elekeza.
Mpogolo
alipiga marufuku vitendo hivyo juzi katika maadhimisho ya siku ya
upandaji miti yaliyofanyika kiwilaya Kijiji cha Nkhoiree Kata ya Iseke
Tarafa ya Ihanja ambapo miti 500 ilipandwa.
Katika
hatua nyingine Mpogolo amewataka viongozi wote wa vijiji kuwa mstari wa
mbele kuhifadhi mazingira katika maeneo yao kwani Ikungi ya miaka 2000
ilikuwa na miti na wanyama na sasa hali inazidi kuwa mbaya na sisi
viongozi na wakala TFS tupo tunaona.
"
Nimewaomba Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) kuchunguza na kuwachukulia
hatua baadhi ya watendaji wao wasio waaminifu. Ninawaalika waje huku
vijijini tufanye mikutano ya hadhara wasikie kilio cha wananchi dhidi ya
utolewaji wa vibali usio halali vya usafirishaji wa mazao ya misitu"
alisema Mpogolo.
Alisema
wananchi wanalalamika kutunza na kuhifadhi misitu yao lakini baadhi ya
watendaji wasio waaminifu wa TFS wanatoa vibali bila kufuata taratibu
ambazo wao wenyewe wamejiwekea kwenye sheria (The Forest Regulation,
2019).
Mpogolo
amewahimiza pia kila nyumba kuwa na mizinga ya nyuki isiyopungua mitatu
kwani kufuga nyuki kunahifadhi mazingira kama sheria ya Uhifadhi ya
Nyuki ya Mwaka 2002 inavyoelekeza. Aidha alisema kufuga nyuki kunaongeza
kipato kwa kuuza asali ambapo mzinga mmoja unaweza kupata zaidi ya sh.
200,000/= kwa mwaka. Ameahidi kuwapeleka kwenye mafunzo vikundi vya
vijana vitakavyokuwa tayari kufuga nyuki ambapo hadi sasa vijana watatu
kutoka Kata ya Issuna wanahudhuria mafunzo ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi
wa wilaya hiyo Justice Kijazi alisema lengo la upandaji miti kwa mwaka
wa fedha 2019/ 2020 ilikuwa ni kupanda zaidi ya miti 500,000 ambapo
mpaka kufikia jana jumla ya miti 280,000 ilisambazwa na kupandwa na
zoezi la usambazaji wa miche hiyo linaendelea.
Kijazi
alisema miti iliyokwisha kupandwa watu binafsi wamepanda miti 208,000,
shule za msingi 37,000, shule za sekondari 20,000 na Taasisi mbalimbali
miti 15,000.
No comments :
Post a Comment