KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais
John Magufuli, katika kikao cha kawaida cha Kamati hiyo kilichoketi leo
Februari. 28, 2020, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba,
jijini Dar esa Salaam, imeazimia kumfukuza uanachama aliyewahi kuwa
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi,
Bernard Membe, kwa kukiuka maadili ya
chama.
Aidha, kamati hiyo imetoa karipio
kwa Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, kwa kukiuka
maadili ya chama huku ikimsamehe Yusuph Makamba kwa makosa kama hayo.
Uamuzi huo umetangazwa na Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, leo Ijumaa Februari 28,
2020, jijini Dar es Salaam.
“Kamati Kuu wa CCM kwa kauli moja
imeazimia kwamba Membe afukuzwe uanachama wa CCM. Uamuzi huu umekuja
baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonyesha mwenendo wake
tangu mwaka 2014 ambapo kwenye chama ameshawahi kupata adhabu nyingine
ambazo zingemsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo.
“Aidha, kamati kuu imepokea maelezo ya Kinana na imeazimia apewe adhabu ya karipio kwa mujibu kanuni za chama,” amesema.
Kuhusu Makamba, Polepole amesema
baada ya kufuatilia kwa kina kumhoji na kumsikiliza na kufuatilia
mwenendo wake, kamati kuu imeazimia mzee Makamba asamehewe.
“Wakati wote tangu aliposomewa
mashtaka yake amekuwa mtu muungwana, mnyenyekevu na mtii kwa mamlaka ya
chama na ameomba asamehewe makosa yake kwa barua na amesamehewa makosa
yake.
“Adhabu ndani ya CCM zinaweza kuwa
siri, akaambiwa mhusika au zikawa za wazi. Adhabu ya karipio inasomwa
hadharani na kufukuzwa inasomwa hadharani,” amesema Polepole.
No comments :
Post a Comment