BONDIA Deontay Wilder atamfukuza
kocha wake Mark Breland baada ya kukasirishwa na kitendo chake cha
kurusha taulo ulingoni Jumapili katika pambano lake dhidi ya Tyson
Fury.
Mmarekani, Wilder alivuliwa taji la WBC uzito wa juu baada ya kuchapwa kwa
Technical Knockout (TKO) raundi ya saba na Fury ukumbi wa
MGM Grand Jijini Las Vegas.Mmarekani, Wilder alivuliwa taji la WBC uzito wa juu baada ya kuchapwa kwa
Na hiyo ni baada ya Breland kurusha taulo ulingoni raundi ya saba kufuatia Wilder kuchapwa ngumi mfululizo bila majibu katika pambano ambalo tayari alikwishaangushwa mara mbili.
Hata hivyo, mbabe wa Alabama, Wilder amesema aliwazuia watu wa kona yake kusalimu amri licha ya kuzidiwa na wamuache aendelee kwa sababu alikuwa ana raundi tano zaidi kuelekea mwisho wa pambano.
Wilder na kocha wake mkuu, Jay
Deas walizungumza na Waandishi wa Habari baada ya pambano na kusema
hawakukubaliana na uamuzi wa kurusha taulo na kwa hilo atabomoa ‘benchi
lake la ufundi’.
Wilder amesema ataanza kushughulikia pambano la marudiano na ataingia na kocha mpya.
“Nimesikitishwa na Mark kwa sababu nyepes tu, tulizungumza juu ya hili mara nyingi na si hasira,” alisema Wilder.
Wilder amesema ataanza kushughulikia pambano la marudiano na ataingia na kocha mpya.
“Nimesikitishwa na Mark kwa sababu nyepes tu, tulizungumza juu ya hili mara nyingi na si hasira,” alisema Wilder.
No comments :
Post a Comment