NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakati wa ziara yake ya siku moja
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mkinga
Yona Mark wakati wa ziara yake katika ni Katibu Tawala wa wilaya ya
Mkinga Joseph Sura
MBUNGE wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dastan Kitandula akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Mark Yona kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM)
Dastan Kitandula wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye
hayupo pichani
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisistiza jambo wakati wa ziara hiyo kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Mkinga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso
NAIBU
Waziri wa Maji Juma Aweso katika akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mkinga
(CCM) Dastani Kitandula kulia na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona
wakitoka kukagua moja ya miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akiteta jamboi na Diwani wa Kata
Mwakijembe kushoto kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna
Mhandisi
wa Wakala wa Maji Vijiji (Ruwasa)
wilaya ya Mkinga Castory Keneth katika akiwa chini ya ulinzi wa askari kufuatia Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuamuru akamatwe kutokana
na kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa maji wilayani humo
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akimsaidia kufunga madumu ya maji
kwenye baiskeli mtoto aliyemkuta akichota maji kwenye bwawa wakati wa
ziara yake wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonawa Wakala wa Maji Vijiji (Ruwasa)
wilaya ya Mkinga Castory Keneth katika akiwa chini ya ulinzi wa askari kufuatia Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuamuru akamatwe kutokana
na kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa maji wilayani humo
NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso
ameliamuru Jeshi la Polisi wilayani Mkinga kumkatama Mhandisi wa Wakala
wa Maji Vijiji (Ruwasa) wilaya ya Mkinga Castory Keneth kutokana na
kushindwa kusimamia mradi wa maji wa Mbuta na kupelekea kushindwa
kukamilika kwa
wakati huku wananchi wakiendelea kutekeseka kupata huduma
hiyo muhimu.
Mradi huo ulianza 2013 ambapo
serikali ilitoa kiasi cha zaidi ya milioni 400 lakini utekelezaji wake
ulishindwa kukamilika na kupeleke tatizo la maji kwenye eneo hilo ambalo
kupata shida ya maji.
Hatua hiyo ilichukuliwa na Naibu
Waziri huo mara baada ya kuutembelea mradi huo ambao ulikuwa
ukitekelezwa na mkandarasi White City ya Jijini Dar es Salaam na
serikali ilikuwa imekwisha kulipa zaidi y a sh.milioni 400 lakini hakuna
kitu ambacho kimefanyika na mkandarasi huyo huku ameutelekeza.
Alisema wizara hiyo imebaba
dhamana kubwa hivyo wataalamu msipokuwa makini mnaweza kuungiza kwenye
matatizo na kuchukiwa na wananchi hivyo kuna haja ya pamoja kufanya
mageuzi ya uzalishaji wa maji vijijini lakini lazima watipie wataalamu
husika.
Naibu Waziri huyo alisema kwamba
lazima Mkurugenzi Ruwasa ajiridhishe kwani wengine hawana sifa na kazi
zao huku akimueleza kwamba mhandisi huyo hatoshi kwenye nafasi hiyo na
hana uwezo ikiwemo kuwa na maslahi kwenye mradi huo.
“Hivyo Mimi kama Naibu Waziri
nimeona kuna ubadhirifu mkubwa hapa hivyo nitatuma timu ya kuhakikisha
ya mabwawa kuja kufanya tathimini kuona namna wanaweza kufanya kazi
hii”Alisema
“Lakini wewe unatetea na kabisa
inaonekana zahiri kuna fedha zimeliwa hapa sasa kabla hatujaenda huko
nimuombe ODC akuchukua ukatusaidia kwenye jambo hilo”Alisema Naibu
Waziri huyo.
Awali kabla ya kutoa maamuzi huyo
Naibu Waziri huyo alimpa nafasi Mhandisi huyo wa Ruwasa kueleza
kuhusiana na mradi huo na namna ulivyotekeleza ambapo alimueleza majibu
yasiyoridhisha na kuamua kuchukua maamuzi hayo.
Hata hivyo serikali imesema kwamba
n kuhakikisha wannahi mkinga wanapata huduma ya maji kwa kuanzisha
mamlaka ya maji pamoja na kupata mradi mkubwa utakaotoa maji Mabayani
hadi Horohoro.
Awali akitoa taarifa ya wilaya
hiyo kwa Naibu Waziri Aweso, Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan
Kitandula alisema kwamba bwawa moja la mbuta lilishazolewa huku
akikabidhiwa mkandarasi aanze kazi upya.
Alisema ilifikia mahali wakatumia
ujanja ujanja kupasua tuta ili maji yasipasue tena tuta lakini eneo la
Mwakijembe umejaa maji kwa hali hii yanaweza kutokea balaa wakati
mwengine hivyo wanahitaji fedha haraka ili mkandarasi akamilishe mradi
kwa sababu kazi ni ndogo.
Aidha alisema lakini wilaya ya
Mkinga hawana mradi mkubwa wa maji hasa kwenye ukanda wa bahari eneo la
mkinga mkoa wa Tanga ambapo ndio lina eneo kubwa kuliko sehemu nyengine
na upozungumzia uwekezaji unaongeleo huku kuwepo mahoteli makubwa lakini
hakuna wekezaji unauofanyika kutokana na ukosefu wa maji.
Hata hivyo alisema kwamba ule
mradi wa mabayani ungeweza kutengewa fedha ufanyika kutoka Tanga mpaka
horohro kilomita 65 na kinachoumiza maji wanayokunywa watu wa Jiji la
Tanga chanzo chake ni Mkinga kata ya Bosha na Mhinduro wanatunza vyanzo
vya maji lakini wao wanabaki watazamaji.
Naye kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Mkinga Yona Mark alisema kwamba wakazi wa wilaya hiyo wanapata
maji bomba, visima na mabwawa kwa asilimia 56 ongezeko hilo ni asilimia
mbili toka asilimia 54 2015/2016.
Alisema kwamba asilimia hiyo
inatokana na kwamba wametengeneza mabwawa lakini hawajatengeneza
miundombinu ya kuwapelekea wananchi maji kwenye maeneo yao .
Alisema wizara ya maji
imewapelekea bilioni 2.9 ili kutekeleza miradi ya maji vijiji vya
mapato,Makao Makuu ya wilaya ya Mkinga Parungu
Kasera,Kilulu,Doda,Bwagamacho,Bamba Mavenegro,Mwarongo,Mbuta na
Mwakijembe.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba
ujenzi wa miradi ya maji vijijini walifanikiwa kupata vyanzo vya maji
tisa badala ya kumi lakini vijiji saba vimekamilisha ujenzi huku miradi
ya miwili ni ule wa Mbuta na Mwakijembe huku akieleza ule wa mbuta
changamoto mkandarasi alikatisha mkataba kwa sababu kutokulipwa.
No comments :
Post a Comment