Waziri wa Afya Hamad Rashid
Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ziara maalum katika
kitengo cha Watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo Hospitali ya
Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid
Mohamed akizungumza na Wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na Maradhi ya
Moyo alipofanya ziara maalum katika kitengo hicho cha Hospitali ya
Mnazi mmoja Zanzibar.
Daktari kutoka Nchini Israel Yifat
Brosh akimfanyia Uchunguzi Mtoto Fatma Mohamed Ali kutoka Jadida Wete
Pemba anaesumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo wakati wa Ziara maalum ya Waziri
wa Afya Hamad Rashid Mohamed katika kitengo hicho cha Hospitali ya Mnazi
mmoja Zanzibar.
****************************
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 31/1/2020.
Serikali ya
Mpinduzi ya Zanzibar inatarajia kujenga Taasisi ya Kitengo cha Maradhi
ya Moyo kata kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati ili kupunguza gharama za
matibabu ya maradhi hayo.
Hayo yameelezwa
na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed wakati alipotembelea
watoto wenye maradhi hayo huko katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Amesema gharama
za matibabu ya maradhi hayo ni kubwa na yanapatikana nje ya nchi hivyo
Serikali imeamua kujenga ili kuwaondoshea usumbufu Wananchi.
Aidha amesema Serikali itaendelea kuwapatia wananchi huduma bora za matibabu bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema uhusiano
nzuri uliodumu kwa miaka 21 baina ya Zanzibar na Israil katika kutoa
matibabau hivyo ni vyema kwa wananchi kuipokea huduma hiyo ili
wafaidike kwani matibabu ya maradhi ya moyo ni makubwa ukilinganisha na
hali za wananchi.
Aidha
amefahamisha kuwa kwa kipindi hiki wataongeza vitanda 1000 kwa wagonjwa
na kutoa mafunzo kwa Madaktari na Manesi wa Hospitali ya Mnazimmoja
ili wananchi waweze kupata huduma bora zaidi kwa wagonjwa wa maradhi
ya moyo.
Waziri Rashid
ameongeza kuwa kwa mwaka huu wameanza matayarisho ya ujenzi wa jengo la
maradhi ya moyo kwa kupeleka wataalamu katika eneo linalotakiwa kujengwa
jengo hilo kwa ajili ya kuangalia mazingira.
Hata hivyo Waziri
wa Afya amewasihi madakatari wanaopatiwa mafunzo hayo kuyatumia vizuri
ili kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.
Kwa upande wa
Daktari anaesimamia kitengo hicho Omar Mohamed Suleiman amesema kuwa kwa
sasa wana wagonjwa 1800 ambao wapo waliobainika kuwa na maradhi hayo
ambapo pia wapo wenye maradhi matibabu mbalimbali ya upasuaji.
Amesema kuwa
kundi la mwanzo waliopatiwa matibabu Israel ni 550 na kila wanapokuja
wataalamu hao wanawafatilia wale waliowafanyia upasuaji wa awali ili
kudumishana ushirikiano kwa wagonjwa na wataalamu hao.
Aidha
amefahamisha kuwa kwa muda wa siku nne wanatarajia kuwachunguza watoto
400 wenye matatizo ya moyo na wakigundulika kuna wana matatizo hayo na
wanahitaji kufanyiwa upasuaji watafanya hatua ya kusafirishwa.
Hata hivyo
amesema wanatarajia kutafuta wahisani kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili
kujua sababu halisi ambazo zinapelekea maradhi hayo.
Nao wazazi wenye
watoto ambao wana maradhi ya moyo wamesema kuwa tatizo kubwa
linalowakabili ni ukosefu wa wa fedha za kununua dawa pindi wanapokwenda
Hospitali kushindwa kumiliki kutokana na hali ngumu ya maisha.
Aidha
wameishukuru Serikali kwa kuwapatia huduma hiyo na kuwataka wazazi wenye
watoto ambao wana maradhi ya moyo kufuata tarehe walizopangiwa kwa
wakati ili kuondosha malalamiko kwa baadhi ya wagonjwa.
No comments :
Post a Comment