
Na. WAMJW-Dodoma
Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa
Haya yamesemwa leo na Waziri wa
Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.
“Ugonjwa huu unasababiswa na
kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019”
(2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo
viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’
mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.
Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia
ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia
ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka
kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili
huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata
maambukizo.
Hata hivyo ametaja dalili za
ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka,
kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu
kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.
“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.
“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.
Wakati huo huo waziri huyo
amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo
kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na
mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi
zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa
kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono
“Kutokana na mwenendo na kasi ya
kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri
kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo
yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi
No comments :
Post a Comment