Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua moja ya nyumba za mradi
wa Nyumba 54 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo wilayani
Masasi mkoa wa Mtwara jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi
wa sekta ya ardhi pamoja na kutembelea miradi ya ujenzi wa NHC. Kushoto
ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba Muungano Saguya.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi wa nyumba 54
za NHC zilizopo wilayani Masasi mkoa wa Mtwara kwa Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi
huo jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha moja ya jalada la
ardhi ambalo utunzaji wake haukufuata taratibu kwa Mkuu wa wilaya ya
Masasi Suleiman Mzee wa pili kushoto, Mbunge wa Jimbo la Masasi Dkt
Rashid Chuachua na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini
Mpoki Mwalufunda (Kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi
wa sekta ya ardhi jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitafuta jalada la ardhi kwa
ajili ya kulikagua katika halmashauri ya wilaya ya Masasi Mjini mkoani
Mtwara jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius
Mtatiro akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na viongozi pamoja na
watendaji wa sekta ya ardhi katika ofisi za Mkuu wa wilaya jana wakati
Naibu Waziri alipotembelea halmashauri ya wilaya ya Tunduru kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi jana. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA
WIZARA YA ARDHI).
****************************
Na Munir Shemweta, WANMM MASASI
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Bodi
ya
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia upya gharama za nyumba zake
ilizojenga maeneo ya pembezoni kwa ajili ya kuziuza.
Dkt Mabula alitoa
kauli hiyo jana wilayani Masasi mkoa wa Mtwara wakati alipotembelea
mradi wa nyumba 54 zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa akiwa
katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika
mikoa ya Kusini pamoja na kutembelea miradi inayofanywa na NHC katika
maeneo mbalimbali nchini.
Kauli hiyo ya
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia
kulalamikiwa na wabunge wa Majimbo ya Masasi Dkt Rashid Chuachua na yule
wa jimbo la Lulindi mkoani Mtwara Jerome Bwanausi kuwa pamoja na
halmashauri kuhitaji nyumba kwa ajili ya watumishi lakini gharama
imekuwa kubwa kiasi cha halmashauri na wananchi kushindwa kuzinunua.
‘’ Ni vizuri bodi
ikae iangalia namna ya kupitia upya gharama za nyumba zote zilizopo
maeneo ya pembezoni kama hizi za Masasi maana zikiachwe bila kununuliwa
itakuwa ni hasara’’ alisema Dkt Mabula.
Naibu Waziri
Mabula alisema, hata kama nyumba hizo zilizojengwa kwa ajili ya kuuza
hazitanunuliwa basi NHC iangaliae namna ya kuzipangisha na kueleza
uhitaji wa nyumba katika eneo la Masasi upo na watumisi wa serikali
wanahitaji kuisha maeneo rafiki.
Hata hivyo,
amezitaka halmashauri nchini kulitumia Shirika la Nyumba la Taifa
kujenga miradi ya nyumba za watumishi kulingana na mahitaji ili kuepuka
kujenga nyumba ambazo mwisho wa siku zinaweza zisinunuliwe.
Kwa upande wake
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya alisema
shirika lake liko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo
uliokuwa umesimama kwa muda ambapo takriban milioni 600 zitatumika
kuukamilisha na kusisitiza imani yake katika kipindi cha miezi sita
ujenzi utakamilika.
Kwa mujibu wa
Saguya, bei inayolalamikiwa ya shilingi milioni 54 kwa nyumba moja
inatokana na gharama kubwa iliyotumiwa na Shirika la Nyumba la Taifa
kuzijenga nyumba hizo na kubainisha kuwa NHC iko mbioni kuzipangisha
baadhi ya nyumba ambazo wananchi wameonesha nia ya kupanga.
Katika hatua
nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula alizitembea wilaya za Nanyumbu na Tunduru na kukagua
utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya hizo.
Dkt Mabula
alibaini utunzaji mbovu wa kumbukumbu za majala ya ardhi pamoja na kiasi
kidogo cha makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi
ambapo aliziagiza halmashauri za Nanyumbu na Tunduru kuongeza kasi ya
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi sambamba na kuzingatia utunzaji
majalada ya ardhi kwa kufuata taratibu ikiwemo kuwepo mawasiliano katika
majalada hayo kutoka afisa mmoja kwenda kwa mwingine.
No comments :
Post a Comment