
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. John Jingu akitoa maelezo kuhusu Sera ya Wazee ya mwaka 2003
ambayo inafanyiwa mapitio ili kuiboresha wakati alipofungua kikao cha
wadau wanaoshughulikia huduma na haki za wazee kwenye ukumbi wa Chuo cha
VETA jijini Dodoma.

Kamishina
wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akitoa akizungumza na wadau
wanaoshiriki kikao cha kukusanya maoni ya kuboresha sera ya wazee ambao
wakati wa ufunguzi wa kikao hicho katika ukumbi wa Chuo cha VETA JIJINI
Dodoma leo.

Mtaalam
mwelekezi wa uandaaji wa Sera ya Wazee Nchini Dkt. Richard Sambaiga
akiongea na washiriki kuhusu kazi ya kukusanya maoni ya kuboresha sera
hiyo kazi inayifanyika kwa kwa muda wasiku mbili katika ukumbi wa VETA
jijini Dodoma.

Baadhi ya
wadau mbalimbali wanaoshiriki kikao kazi cha kuhuisha Sera ya Wazee
wakifuatilia mwongozo wa utoaji maoni ili kuboresha sera hiyo katika
ukumbi wa VETA jijini Dodoma.
………………….
Mwandishi Wetu,Dodoma
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na
watoto Dkt. John Jingu amewataka wadau wa utoaji huduma kwa wazee kutoa
maoni ya kuboresha Sera ya
Taifa a Wazee ya Mwaka 2003 ili kukidhi
mahitaji ya wazee ambao wamelitumika Taifa kwa bidii na maarifa pindi
walipokuwa na nguvu na sasa wanapata huduma, fursa na kuenziwa.
Dkt. Jingu
alisema hayo wakati wa kufungua Kikao cha wadau wa Kitaifa waliokutana
jijini Dodoma kwa lengo la kuhuisha Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003
ambayo inapitiwa, kujadiliwa na kupokea maoni kuhusu uhalali wa matamko
na maelekezo ya kisera kwa ajiliya kuboreshwa ili kuwapa fursa ya
kuendelea kutoa mchango katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa
ujumla.
Aidha
Dkt. Jingu amebainisha kuwa Mtaalam mwelekezi Dkt. Richard Sambaiga
ameandaa rasimu ya awali ya Sera hiyo itatumika kuchochea fikra za wadau
ili kupata maoni chanya yatakayojumuishwa katika Sera iliyoboreshwa
maana itazingatia mazingira halisi ya afya, ulinzi, usalama, hifadhi ya
kijamii, matunzo na ushirikishwaji katika masuala ya kijamii.
Katika
kutkeleza Sera ya Wazee ya Mwaka 2003, Dkt. Jingu ameeleza kuwa Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhudumia wazee ikiwa ni pamoja
na kusimamia makao ya wazee 17 ya yanayomilikiwa na Serikali ambayo
hivi sasa yamepunguzwa manne na kubaki 13 kwa ajili ya kuboresha huduma
kwa wazee wasiojiweza wanaoishi katika makao hayo baada ya familia zao
kushindwa kuwapa huduma za msingi.
’’Katika
mazingira ya kawaida Serikali inachukua jukumu la kuwalea wazee baada ya
kuthibitika kuwa familia husika haina uwezo au haikujitokeza kutoa
huduma’’. Aliongeza Dkt. Jingu.
Aidha
Dkt. Jingu amesisitiza kuwa wajibu wa kulea wazee wasio jiweza sio
haukomei tu kwa familia bali ni jukumu linalohussha pia jamii kwa ujumla
hivyo amewataka wadau wote kutambua kuwa kila mtu anamchango katika
malezi na matunzo ya wazee hapa nchini.
Kadhalika,
Mpango wa utambuzi wa wazee katika Halmashauri hadi kufikia Desemba,
2019 umewezesha kuwatambua jumla ya Wazee 1,837,162 (Me 834,595 na Ke
1,002,567). Kati yao wazee wasio na uwezo 684,383 (ME:348,171,
KE:336,212) wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bila malipo.
Naye
Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi ameeleza kuwa ni
muhimu kuboresha Sara ya wazee ili kuakisi mahitaji na changamoto
zinazowakabili wazee kwa kuatika mazingira ya sasa maana sera iliyopo ni
ya miaka16 iliyopita.
Dkt. Ngondi
ameongeza kuwa azma ya kikao cha wadau wanaosimamia na kushughulikia
masuala ya huduma na haki za wazee watajadili kwa pamoja na na
kupendekeza namna sera pendekezi itaweza kuzingatia maeneo ya msingi.
Aidha
Mtaalam mwelekezi anayeandaa Sera ya Wazee Dkt. Richard Sambaiga
aliwambia washiriki kuwa suala la uzee na kuzeeka sio suala la kupuuzwa
tena bali ni jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa katika mipango ya
maendeleo ya kisekta maana idadi ya wazee hapanchini ambayo ni takriban
asilimia 5.6 itaongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2050 maana uwekezaji
unaofanyika unaongeza idadai ya wazee na kupunguza umasikini
uliokithiri.
Itakumbukwa
kuwa wazee wanatambulika kuwa ni walinzi wa mila na desturi,
washauri/wapatanishi, na walezi wa watoto wadogo hivyo Sera
inayoboreshwa itaweka matamko ambayo yatahakikisha wazee wanathaminiwa
katika jamii kwa kuwa, uwepo wa Taifa la Tanzania ni kielelezo tosha
cha mchango mkubwa wa utumishi wa wazee katika nyanja mbalimbali.
No comments :
Post a Comment