*******************************
KAMATI ya Utendaji ya Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) , inawahimiza
wanachama wake ambao wana nia ya kushiriki Mkutano Mkuu Maalum wa chama
hicho kuhakikisha wanathibitisha kwa maandishi ili waweze kuhudhuria
mkutano huo.
Hatua hiyo inatokana na mwitikio
mdogo wa waliothibitisha kushiriki, hivyo kufanya
maandalizi mengine ya
mkutano huo kushindwa kufanyika vizuri.
Kwa mazingira hayo mwisho ya
kuthibitisha kushiriki itakuwa Jumatatu Januari 13 mwaka huu, na mkutano
huo sasa utafanyika Jumapili Januari 19 na hakutakuwa na muda wa ziada
kwa watakaoshindwa kuthibitisha.
Lengo la mkutano huo ni kujadili
masuala mbalimbali ya chama, ambapo pia utapokea taarifa kutoka Kamati
ya Marekebisho ya Katiba iliyoundwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
na pia utapokea mapendekezo kutoka Kamati ya Utendaji ya
TASWA inayomaliza muda wake.
Watakaohudhuria Mkutano Mkuu
Maalum ni wanachama wote walio katika leja baada ya kushiriki uchaguzi
wowote wa TASWA kuanzia mwaka 2004, 2007, 2010, 2014 na wanachama wapya
wote walioingia kuanzia mwaka 2015 hadi Juni mwaka jana.
Kwa mazingira hayo ili mkutano
ufanyike kwa ufanisi ni vyema yeyote mwenye nia ya kushiriki athibitishe
kwa maandishi akitaja jina lake na chombo na kutuma kwa email: taswatz@yahoo.com au mgosius@yahoo.com au machagift@gmail.com, ili taratibu nyingine ziendele.
No comments :
Post a Comment