Jengo jipya la Benki ya Watu wa
Zanzibar PBZ lililowekwa Jiwe la msingi na Rais Mstaafu wa awamu sita Dk
Aman Abed Karume Malindi (MOTOR TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra
za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Dk
Aman Abeid Karume akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la
Msingi Jengo jipya la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR
TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Dk
Aman Abeid Karume akikata utepe katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la
Msingi Jengo jipya la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR
TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar,
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya
Watu wa Zanzibar (PBZ)Juma Ameir Hafidhi akitoa maelezo kuhusu Ujenzi
katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya la Benki ya Watu
wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra
za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Waziri wa Fedha na Mipango Balozi
Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi
katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya la Benki ya Watu
wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra
za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Dk
Aman Abeid Karume akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la
Msingi Jengo jipya la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR
TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Dk
Aman Abeid Karume katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
mbalimbali katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya la
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Malindi (MOTOR TRADE)Zanzibar.Ikiwa ni
shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
………………
Na Khadija Khamis ,Maelezo Zanzibar
Rais Mstaafu wa
Zanzibar wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alisema kuimarisha
huduma ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutasaidia ukuaji wa uchumi
nchini.
Aliyasema hayo
alipokuwa akizungumza katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la
jengo la Benki ya Malindi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya kutimiza
miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema kuimarisha huduma za kibenki kwa kutumia njia za kiteknolojia kutawarahisisha wateja kupata huduma zao kwa haraka .
Aidha alisema
hatua za Serikali kujenga matawi mbali mbali ya kutoa huduma za kibenki
kutasaidia kuepusha msongamano wa wateja pamoja na kuwarahisishia kupata
huduma zao kwa haraka .
Alisema Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ikitumia benki hiyo kwa ajili ya
shughuli za kiserikali lakini baada ya kuona benki nyingi
zinabinafsishwa ikaanzishwa benki ya watu wa Zanzibar ili kuwaondoshea
usumbuvu wananchi wake.
Aliwataka
wafanyakazi wa benki hiyo kuwa makini katika utekelezaji wa kazi zao
kwani kufanya hivyo kutasaidia kuepusha migogoro kwa wateja wao .
Hata hivyo
aliwataka wateja ambao wanapatiwa mikopo kulipa kwa wakati na utaratibu
uliopangwa ili na wateja wengine waweze kupata kuduma hiyo .
Nae Waziri wa
Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amesema ongezeko la
kiwango kikubwa cha gawio na kodi ya mapato katika huduma za kibenki
kutaimarisha ukuwaji wa uchumi kwa haraka .
Alisema lengo kuu
la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia maendeleo wananchi
wake na kuwapunguzia makali ya maisha kwa njia ya mikopo .
Mapema Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Juma Ameir Hafidh,
alisema, kukamilika kwa jengo hilo, kutaweza kukidhi mahitaji ya kibenki
kwa wakati wa sasa na baadae.
Aidha alisema
kuwa, utayarishaji wa michoro na usimamizi wa ujenzi huo unafanywa na
mshauri elekezi ambae ni kampuni ya NEDCO kutoka Dar-es Salaam.
Alisema kuwa
jengo hilo, litakuwa ni la ghorofa moja (G+M) na lina sehemu mbili
ambazo ni sehemu ya jengo jipya na sehemu ya jengo la zamani, ambapo
sehemu ya jengo hilo, sehemu ya chini kutakuwa na matawi pacha ya benki
ya kawaida na benki ya huduma za kiislamu, na pia kutumiwa na maafisa
wote waliopo jengo la darajani na jengo la mpirani.
Alifahamisha kuwa
ujenzi huo ulichelewa kutokana na kuchelewa kupatikana kwa mchanga na
mawe katika ujenzi, taratibu ndefu za upatikanaji vibali katika kila
hatua ya ujenzi katika maeneo ya hifadhi ya mji mkongwe.
Alisema sababu
nyengine ni tatizo la kuhamisha drainage system ambayo imekata
katikati ya jengo, tatizo la kuhamisha umeme ambao umepita chini ya
ardhi pamoja na mabadiliko ya jengo ili kuweza kuhudumia baadhi ya
wafanyakazi.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo, unatarajiwa kumalizika April 2020.
No comments :
Post a Comment