Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza majina ya Viongozi
mbalimbali walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 31,
2020.
Wizara.
1.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bi. Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa
Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua
nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.
2.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu.
3.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Prof. Riziki Silas Shemdoe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala
Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye
amestaafu.
4.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bi. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya
uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua
nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.
5.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
6.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Leonard R. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla
ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati
Mbadala.
Mikoa.
1.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bi. Judica Haikase Omari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga.
2.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Stephen Mashauri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
3.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Majeshi.
1.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.
Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye
ameteuliwa kuwa Balozi.
2.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Naibu Kamishna wa Magereza (DCP)
John William Masunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
DCP John William Masunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi
wake umetenguliwa.
Ardhi.
1.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Nathaniel Mathew Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Nathaniel Mathew
Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
Mahakama.
1.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Wilbert M. Chuma kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
2.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Kelvin D. Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
3.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bi. Shamira S. Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
==========
4.
Mhe. Rais Magufuli
amewateua Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika, Wakili - Julius Kalolo
Bundala na Wakili
– Genoveva M. Kato kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Tarehe
ya kuapishwa kwa viongozi hawa itatangazwa baadaye.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Dar
es Salaam
No comments :
Post a Comment