Waziri
Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda
amezindua kitabu cha “MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY” kilichoandikwa na
mwanahabari nguli na mtaalamu wa masuala ya kiuchumi, Bw. Derek Murusuri.
Kitabu hiki kinashajihisha Waafrika kufikiri
na kutekeleza mageuzi endelevu yatakayoifanya Afrika kuwa ni Bara lenye nguvu
kubwa ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa mtunzi wa kitabu hicho Bw. Derek
Murusuri, kabla ya kuandika kitabu hicho alifanya utafiti kwa takriban miaka 21 na kwamba maudhui
yaliyomo ndani ya kitabu hicho yataleta mabadiliko katika Afrika ijayo.
Uzinduzi huo umefanyika Januari 29, 2020 jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe.
Mizengo Kayanza Peter Pinda, akizunguzma wakati akizundua kitabu cha "MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY" jijini Dar es Salaam Januari 29, 2020.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe.
Mizengo Kayanza Peter Pinda, akimpongeza mtunzi wa kitabu hicho, Bw.
Derek Murusuri mara baada ya kukizindua.
Balozi Christopher Liundi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Bw. Derek Murusuri akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mtangazaji mkongwe nchini, Bw. Jacob Tesha akitoa nasaha zake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw.Frederick Ntobi, akizungumza







No comments :
Post a Comment