Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyenyoosha mkono), akimuuliza swali
Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho, Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA), Alphonce Malibiche baada ya kutembelea kituo cha
kanzidata kilichopo Kibaha mkoani Pwani, lengo la ziara hiyo ni
kuhakikisha utolewaji wa namba na vitambulisho vya taifa ili
kwenda sambamba na siku zilizoongezwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa
wananchi kupata vitambulisho hivyo ili waweze kusajili laini za
simu.Wanne kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Anold Kihaule.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji
Vitambulisho, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Alphonce
Malibiche akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia),juu ya hatua zinazofuatwa katika
kukagua taarifa za muombaji kitambulisho kabla akijazalishwa wakati wa
ziara ya naibu waziri kutembelea kituo cha kanzidata kilichopo Kibaha
mkoani Pwani. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Anold
Kihaule Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
************************************
Na Mwandishi Wetu
Katika kwenda
sambamba na siku 20 zilizongezwa na Rais Dkt.John Magufuli wakati
akisajili
laini yake ya simu kwa alama za vidole Desemba 27,2019 mjini
Chato mkoani Geita,Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) wametakiwa
kuongeza idadi ya watumishi katika kituo cha kuchakata taarifa za
waombaji nchi nzima kilichopo Kibaha mkoani Pwani ili kuhakikisha kila
mwananchi anayekidhi vigezo kupata Kitambulisho cha Taifa ili aweze
kusajili laini yake ya simu.
Akizungumza baada
ya kutembelea kituo hicho Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt.
Anold Kihaule kuongeza idadi ya watumishi katika kituo hicho na kuongeza
pia masaa ya kufanya kazi kutoka nane mpaka kumi na sita ili
kuhakikisha wananchi wanapata namba na vitambulisho baada ya nyongeza ya
siku 20 ziliyotolewa na Rais Magufuli.
“Nimetembea
katika vituo mbalimbali vya NIDA nchi nzima,changamoto kubwa wanayotoa
wananchi ni kwenda kila siku kufuatilia kitambulisho au namba katika
kituo husika lakini wamekua wakipata majibu kwamba bado kipo kwenye
mchakato,wakati mwingine ameomba miaka mitatu iliyopita sasa anapoteza
muda na gharama kufuatilia kitambulisho lakini nimetembelea hapa leo
nimegundua uchache wa watumishi,mkurugenzi ongeza watumishi hapa..”
alisema Masauni
“……naomba pia
ongeza muda wa kufanya kazi,kutoka masaa nane mpaka kumi na sita,Rais
ashasema muda hautaongezwa wa usajili laini za simu,sasa wananchi
wanafurika na kupata taabu vituoni huko,sisi ndio wawakilishi wao lazima
tuwasemee na mkuu wa nchi ashatoa maelekezo sasa ni utekelezaji tu”
aliongeza Masauni
Akizungumza
katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Anold Kihaule alisema
watayatekeleza maagizo hayo ya serikali huku akiwaasa wananchi ambao
tayari wana namba za utambulisho waende kusajili laini zao ili kwenda
sambamba na muda ulioongezwa na Rais Dkt. Magufuli.
“Jumla ya watu
milioni 7.6 tayari wana namba za utambulisho nchi nzima na kila siku
tunaendelea kutoa namba hizo sehemu mbalimbali nchini na mnaweza kuona
kwa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja tunatoa namba pale nani
zoezi la siku zote za wiki,hatuna sikukuu wala siku za mwisho za wiki”
alisema Dkt.Kihaule
Kila mmiliki wa
simu ya mkononi anatakiwa kusajili laini yake kwa alama za vidole kwani
kutofanya hivyo itamaanisha kutoweza kupiga wala kupokea simu,vile vile
muhusika hatoweza kutuma wala kupokea ujumbe mfupi wa maneno.
No comments :
Post a Comment