Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akisalimiana na baadhi ya Maofisa
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kabla ya kukagua ujenzi wa Makao Makuu
ya Jeshi hilo ambao unaendelea jijini Dodoma.
Mratibu na Msimamizi Mkuu wa
miradi ya ujenzi ambayo inatekelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
jijini Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Costantine Kiwone,
akimweleza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (katikati) na
Maofisa wengine hatua mbalimbali za ujenzi wa nyumba za askari, Makao
Makuu ya Polisi na makazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) jijini Dodoma
jana.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (katikati), akitoa maelekezo kwa
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka
Semwanza (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu, Emmanuel
Kayuni (wa pili kulia) baada ya kufanya ukaguzi katika ujenzi wa majengo
ya jeshi hilo jijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamhanga.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia), akiwa na Wakurugenzi na
Maofisa wa Wizara hiyo akisisitiza jambo kwa Maofisa wa Usajili wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mkoa wa Dodoma, alipofanya
ziara ili kuangalia utendaji kazi na huduma zinavyotolewa kwa wananchi.
PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA
No comments :
Post a Comment