Mkurugenzi Kinga na Elimu ya
Afya Dk,Fadhill Mohamed Abdalla akisisitiza jambo wakati akizungumza na
Waandishi wa Habari kihusiana na Tahadhari zilizochukuliwa kujikinga na
Maradhi ya Corona yaliozuka katika Nchi ya China hafla iliofanyika
Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya
Dk,Fadhill Mohamed Abdalla akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana
na Tahadhari zilizochukuliwa kujikinga na Maradhi ya Corona yaliozuka
katika Nchi ya China hafla iliofanyika Ofisini kwake Wizara ya Afya
Mnazimmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
*****************************
Na Rahma Khamis Maelezo 29/1/2020
Wananchi
wametakiwa kufika katika Vituo vya Afya kwa ajili ya uchunguzi na
kupatiwa
matibabu mara watapobaini kuwa na mafua na homa kali ili
kujikinga na maradhi ya Corona yaliyojitokeza nchini China hivi
karibuni.
Hayo yameeleza
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Mohamed Abdallah huko
Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja wakati aliopokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na maradhi hayo.
Amesema dalili ya
maradhi hayo ni kuhisi mafua na homa ambayo baadae huzidi hatimae
kupata homa kali, vidonda vya mdomo na kwenye mishipa ya koo pamoja na
homa ya mapafu.
Mkurugenzi huyo
amewasisitiza wananchi kufuatia taarifa zinazotolewa katika vyombo vya
habari kuhusiana na maradhi hayo ili kuepuka uzushi katika jamii na
kuishi kwa amani kutokana na hali ya maradhi ilivyo nchini.
Dkt Fadhil
amefahamisha kuwa kirusi cha maradhi hayo kipo toka zamani lakini kwa
sasa kimezuka kirusi chengine kipya kinachoitwa Novel Corona Virus
ambacho kinatokana na jamii hiyo na kinaenea kwa kutumia njia ya hewa.
Mkurugenzi huyo
ameeleza kuwa wameongeza nguvu za ziada katika maeneo ya Uwanja wa Ndege
na Bandarini kwa kuwapa mafunzo maafisa wa vitengo hivyo pamoja na
kuweka vifaa maalum vya kutumia katika Hospitali ya Mnazi mmoja pindi
yakigundulika maradhi hayo ili kuweza kudhibiti yasienee nchini.
“Lakini pia
tumeandaa eneo maalum huko Fuoni Kibondeni kwa ajili kuwaweka wagonjwa
pindi tu tukigundua kuwa mgonjwa amejitokeza na maradhi hayo, na pia
tunatoa mafunzo katika vituo vya afya jinsi ya kuhudumia wagonjwa na
kutoa fomu maalum kwa wageni wote wanaotoka nchi ambazo zimegundulika
kuwa na maradhi hayo na tutawafatilia kwa muda wa siku 14 ili kupata
taarifa zake”, alisema Dkt Fadhil.
Amefahamisha kuwa
Serikali imejipanga kwa ajili ya kujikinga na maradhi hayo tayari
imeshaunda timu sita ili kufuatilia wagonjwa wanaopata maradhi hayo na
kuwapatia mafunzo pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya
habari kuhusu ugonjwa huo.
Akizungumzia
kuhusu maradhi ya Malaria Dkt Fadhil amesema kuwa katika jamii kuna mbu
wanaosababisha maradhi hayo hivyo amewataka wananchi kuchua tahadhari
kwa kuweka mazingira safi pamoja kutumia vyandarua vyenye dawa ili
kujikinga na maradhi hayo.
No comments :
Post a Comment