Wednesday, January 1, 2020

MBUNGE PROFESA MUHONGO AKABIDHI ZAWADI ZA VIKOMBE, FEDHA KWA WASHINDI WA KUPIGA KASIA MUSOMA VIJIJINI


 Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo akimkabidhi zawadi  ya Kombe la ushindi katika mashindano ya kupiga kasia yaliyofanyika katika Ziwa Victoria Kijiji cha Bukima,Musoma Vjijini mwishoni mwa mwaka 2019.
 Mmoja wa washindi wa mashindano hayo (kulia), akipongezwa kabla ya kukabidhiwa kombe la ushindi wa mashindano ya hayo ya kupiga kasia.
 Mmoja wa washindi akikabidhiwa zawadi ya Kombe huku akiashangiliwa na wenzake.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo
 Wananchi wakishuhudia mashindano hayo.

Na Mwandishi Maalumu
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amekabidhi zawadi za vikombe na fedha taslimu kwa washindi wa mashindano ya Kupiga Kasia (The Annual Boat Race) yaliyofanyika mwishoni mwaka jana katika Kijiji cha Butima, Ziwa Victoria jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameamua kwa vitendo kufufua  Utamaduni na Michezo jimboni mwao iliyokuwa inafifia  na
kuanza kutoweka., ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya  CCM 2020, jimboni humo. 
 
Kila Mwaka, Mbunge huyo anatayarisha na kufadhili MASHINDANO ya KWAYA (nyimbo) na NGOMA ZA ASILI.
 
Vilevile, Mbunge huyo ni mmoja wa WAFADHILI wa Timu ya Mpira ya Mkoa wa Mara, BIASHARA UNITED inayoshiriki Ligi Kuu ya Taifa. Ameombwa na kukubali
kuna mmoja wa Wafadhili wa WASAGA FC ya Kata ya Nyamrandirira itakayoshiriki Ligi ya Daraja III. Mbunge huyo alishagawa Vifaa vya Michezo Vijijini na Mashuleni.
 
MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (The Annual Boat Race) – Washindi na Zawadi Mbunge wa Jimbo ametoa ZAWADI hizi:
 
MSHINDI 1
Kata ya Murangi
Tsh Milioni 1 & Kikombe
 
MSHINDI 2
Kata ya Musanja
Tsh 700,000 & Kikombe
 
MSHINDI 3
Kata ya Suguti
Tsh 400,000 & Kikombe
 
Mshindi wa Nne
Kata ya Bukima
 
Mshindi wa Tano
Kata ya Rusoli
 
ZAWADI ndogo ndogo nazo zilitolewa.
 
Wananchi
wa Jimbo la Musoma Vijijini wameomba Mbunge wa Jimbo lao AENDELEE
kutayarisha MASHINDANO ya kupiga KASIA na ikiwezekana yafanyike mara
pili kwa Mwaka.
 
Picha
zilizoambatanishwa hapa zinaonesha MATUKIO mbalimbali ya Mashindano ya
kupiga Kasia yaliyofanyika Kijijini Bukima, jana, tarehe 30.12.2019.
 
SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO
 
“MWAKA MPYA (2020) uwe ni Mwaka wa Maarifa mapya, Ubunifu mkubwa, Ushirikiano mkubwa, na Utekelezaji wenye umakini na ufanisi mkubwa.

No comments :

Post a Comment