Walimu wakuu washule mbalimbali za
msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakikagua madarasa
yanayojengwa wakati wa ziara na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo
Kiduma Mageni.
Muonekano wa madarasa yanayojengwa.
Muonekano wa madarasa yaliyojengwa
na kukaribia kutumika kwa wanafunzi wa shule za msingi katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Mmoja wa walimu wakuu waliokuwa
katika ziara hiyo, akieleza mbele ya walimu, Afisa Elimu mwenendo wa
ujenzi wa madarasa katika shule yake ulipofikia.
***********************************
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na
ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157
kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainisha na Afisa elimu
msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa
ziara ya kukagua
miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya
miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account.
Akizungumza mara baada ya
kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni alisema kuwa katika fedha hizo
zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na
matundu ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo
ya ndani, shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu
kupitia mpango wa EP4R.
Aidha Mageni ameongeza kuwa katika
fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726 ni pesa kutoka
mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, na
kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu za
wananchi.
Sambamba na hivyo, ndugu Mageni
amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42 na
kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa vimeanza kutumika na wanafunzi huku
vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia 95.
Mageni amesema Halmashauri ya
Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na Mkuu wa Wilaya
Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa
inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika
mazingira mazuri.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu
ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa elimu bure
na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo
wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo.
“ Niwapongeze sana kwa kazi nzuri
wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi wanakaa kwenye majengo
mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na
muda sio mrefu yatakabidhiwa ili watoto wetu wa anze kuyatumia.
“Nampongeza sana Mhe. Chongolo,
Kagurumjuli na timu yake yote wanafanya kazi kubwa, inaonekana, Rais
wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio kwamba
tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto
wetu wasome kwenye majengo safi” alisema Mageni.
Mageni amesema ameridhishwa na
ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka walimu hao kuwa
wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo.
Kwa upande wa mwalimu hao
waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa
kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa
nafasi.
Mmoja wa walimu hao ambaye ni
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge alisema kuwa elimu
bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa wazazi na hivyo
kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake amejengewa
vyumba nane vya madarasa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na matundu 13 ya
choo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa
kuwapatia majengo hayo.
Hata hivyo walimu hao wameonyesha
kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika shule zao,
sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya
Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo.
No comments :
Post a Comment