
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), akiwa na viongozi waandamizi wa
Wizara hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao
kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa mwaka
wa fedha 2018/19, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni CPA Aziz Kifile (Mhasibu
Mkuu Msaidizi wa Serikali), Bw. John Sausi (Mkurugenzi wa Idara ya
Mifumo ya Usimamizi wa Fedha), CPA Francis Mwakapalila (Mhasibu Mkuu wa
Serikali), Bi. Mary Maganga (Naibu Katibu Mkuu), CPA Pius Maneno
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), na
CPA Evansi Asenga (Mkuu wa Hazina Ndogo Dar es Salaam)

Meza Kuu wakiwa
katika picha ya pamoja na wahasibu (CPAs) wanawake wakati wa ufunguzi wa
kKikao Kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za Serikali kwa
mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza katika hafla ya
ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa taarifa za hesabu za majumuisho za
Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya
wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa taarifa za Hesabu za Majumuisho za
Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, kilichofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
******************************
Ramadhani Kissimba na Josephine Majura, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ameiagiza Menejimenti ya
Wizara ya Fedha na Mipango kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahasibu
wote wanaofanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya
uhasibu kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi na rushwa.
Dkt. Mpango
alitoa maagizo hayo wakati akifungua Kikako Kazi cha kuandaa Hesabu za
Majumuisho za Serikali za mwaka 2018/19 pamoja na kuzindua Mfumo mpya wa
uandaaji wa taarifa za fedha za Majumuisho (Government Accounting
Consolidation System (GACS), Jijini Dar es Salaam
Dkt. Mpango
aliwataka wahasibu wote nchini kuwa wazalendo na kusimamia ipasavyo
matumizi ya rasimali za Umma na kuwataka kuhakikisha kuwa usalama katika
Mifumo ya Fedha unakuwa madhubuti ili kuondoa uwezekano wa mifumo hiyo
kudukuliwa na kuleta hasara kubwa kwa Serikali na Wananchi.
Aidha Dk. Mpango
alimpongeza Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Francis Mwakapalila, pamoja na
Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha Bw. John Sausi kwa kuonesha dhamira na nia
ya kweli ya kuhakikisha wanatengeneza Mifumo bora ya kifedha ili kuleta
ufanisi mkubwa katika kukusanya na kuhasibu mapato na matumizi ya
Serikali.
Aliongeza kuwa
dhamira hiyo imedhihirika kwa kuanzisha Mifumo ya Kifedha ya kimtandao
kama Government e-payment Gateway (GePG), Government Salary Payment
Platform (GSPP), na sasa Government Accounting Consolidation System
(GACS).
‘’Nimefurahi sana
kuona kwamba ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne tangu Serikali ya
Awamu ya Tano iingie madarakani, mmeanzisha Mifumo mingi na madhubuti ya
kukusanya Mapato na Maduhuli ya Serikali, pamoja na Mifumo ya kuhasibu
rasilimali za umma yenye kukidhi viwango vya kimataifa” alisema Dkt.
Mpango.
Aliongeza kuwa
ni ushahidi bayana kuwa, watendaji hao wanatafsiri kwa vitendo dhamira
na dira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi shupavu wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya Wananchi hasa Wanyonge.
Pia alieleza kuwa
matarajio ya Serikali ni kwamba mfumo huu ulioanzishwa pamoja na
Mifumo iliyokwisha kuanzishwa itaitumika vizuri kwa weledi na uadilifu
mkubwa katika kutoa huduma bora kwa Wananchi na ikizingatiwa hilo
matarajio ya wananchi na rasimali za umma zitatumika ipasavyo kuboresha
Maisha yao.
Awali Mhasibu
Mkuu wa Serikali CPA. Fransis Mwakapalila alisema hatua ya kuandaa
Hesabu za Majumuisho kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki unaifanya
Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutayarisha Hesabu za
Majumuisho kwa kutumia mfumo uliandaliwa na wataalamu wake wa ndani
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
CPA. Mwakapalila
alisema kwa sasa Tanzania ni nchi inayoongoza kwa ubora wa Taarifa za
FeFha za Majumuisho (CFS) zenye kukidhi viwango vya Kimataifa katika
sekta ya Umma (IPSAS) Barani Afrika.
Akizungumza
katika kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa
fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, amesema Idara
yake itaendelea kujenga mifumo ya kielektroniki ya fedha ili kuhakikisha
makusanyo ya pesa za Serikali yanapita katika mifumo sahihi.
“Mafanikio
yanayopatikana katika uandaaji wa mifumo hii yanatokana na watalaamu
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi
yao, na wataalamu hao wamekuwa wakiandaa mifumo mbalimbali ukiwemo
mfumo wa kukusanya maduhuli ya Serikali kwa njia ya Mtandao (GePG)
ambapo Taasisi zaidi 616 zimeshaunganishwa kwenye mfumo huo.
Bw.Sausi alisema
kuwa mfumo mpya wa uandaaji wa taarifa za fedha za majumuisho (GACS)
ambao umezinduliwa na Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango utasaidia kupunguza
utiriri wa kuwa na mifumo mingi ya uandaaji wa taarifa za fedha.
No comments :
Post a Comment