
Mkurugenzi wa Huduma Za Maabara
wa TMDA, Dkt. Danstan Hipolite akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya
TMDA waliotembelea Maabara hiyo ya Kanda ya Ziwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMDA, Balozi, Dkt. Ben Moses (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
………………………………………….
BODI ya Ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).
BODI ya Ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).
Katika ziara hiyo, Bodi hiyo
imeweza kujionea utendaji kazi za udhibiti wa ubora, usalama na
ufanisi
wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika maabara kubwa nacya kisasa
iliyojengwa kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma kwa
wananchi.
Aidha, bodi hiyo imeweza kufanya kikao chake cha kawaida, ikiwa ni cha kwanza kwa mwaka 2020.
Sambamba na hilo Bodi imekutana
na watumishi wa TMDA kanda ya Ziwa ambapo Mwenyekiti wa MAB, Mhe.
Balozi, Dkt. Ben Moses amewapongeza Menejimenti naxwatumishi kwa
mafanikio ya utendaji kazi yaliyofikiwa na kuwahimiza kuendelea kujituma
na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuwezesha taasisi kufikia lengo
lake la kuendelea kulinda afya ya wananchi kwa ufanisi zaidi.
Ziara ya wajumbe wa MAB
inahusisha pia kutembelea na kujionea changamoto za udhibiti katika
vituo vya Forodha vya Sirari na Mutukula.
No comments :
Post a Comment