Sunday, January 19, 2020

BODI NISHATI VIJIJINI YAWABANA WAZALISHAJI NYAYA ZA UMEME


 
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Julius Kalolo,akiongoza kikao na wazalishaji wa nyaya za umeme alipofanya ziara ya siku moja kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme vya Kilimanjaro Cables, MCL na Europe Industries (Tropical) vilivyopo Dar es Salaam.
Viongozi wa  Bodi ya Nishati Vijijini (REB), wakimsikiliza mmoja wa wazalishaji wa nyaya za umeme walipofanya ziara ya siku moja kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme vya Kilimanjaro Cables, MCL na Europe Industries (Tropical) vilivyopo Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Julius Kalolo,akisalimiana na Mkurugenzi wa Europe Industry Bw.Charles Mlawa wakati wa ziara ya kukagua na kujionea viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme vya Kilimanjaro Cables, MCL na Europe Industries (Tropical) vilivyopo Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Julius Kalolo (kushoto) akimsikiliza mdau (katikati), wakati wa ziara ya kukagua na kujionea viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme vya Kilimanjaro Cables, MCL na Europe Industries (Tropical) vilivyopo Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangira
………………
Na.Alex Sonna,Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Julius Kalolo ameagiza wazalishaji wa nyaya za
umeme zinazotumika katika Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza (REA III) kukamilisha usambazaji katika maeneo yote kabla ya utekelezaji wa mradi mwezi Februari, mwaka huu.
Agizo hilo alilitoa katika ziara ya siku moja 18/01/2020 kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme vya Kilimanjaro Cables, MCL na Europe Industries (Tropical) vilivyopo Dar es Salaam.
Amesema wakandarasi wanadai kuwa wazalishaji wanashindwa kuzalisha nyaya kwa muda unaotakiwa kutokana na kuwa na zabuni nyingi.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa changamoto kubwa katika utekelezaji wa REA III hivi sasa ni kukosekana kwa nyaya ambazo zinahitajika kuwekwa ili kuwezesha wananchi kupata huduma ya nishati ya umeme.
“Kwa upande wa Tropical na MCL wanasema wana oda za kutosha hivyo hawawezi kupokea kwa muda huu mfupi oda mpya na kuzalisha kwa muda mfupi, lakini zile oda walizokuwa nazo wamesema hadi kufikia mwezi wa februari watakuwa wamewapa wakandarasi ili wamalizie mradi,”amesema
Aidha, amesema Tropical wanasema hawana oda kutoka kwa wakandarasi wa REA zaidi ya Tanesco.
“Nyaya zipo lakini tatizo ni wakandarasi wetu, tunalishughulikia maana wanatatizo la kurundikana kwa mzalishaji au msambazaji mmoja,”amesema
Naye, Mkurugenzi wa Europe Industry Bw.Charles Mlawa ametoa rai miradi inayotekezwa kwa mradi huo nyaya na transfoma zipo za kutosha na miradi itakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangira, amesema katika maeneo ya vijijini waliyotembelea wamebaini nguzo kusimama kwa muda mrefu na taarifa zilizopo tatizo ni nyaya.
Kadhalika, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amosi Maganga, amesema baadhi ya wakandarasi kurundikana kwa msambazaji mmoja wakati maeneo mengine yana nafasi ya kutosha.
Pia amesema mradi huo ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka jana lakini kutokana na sababu mbalimbali baadhi ya wakandarasi wapo asilimia 98 ya utekelezaji wengine 100 ni imani yangu kwa kipindi kilichobaki watakamilisha

No comments :

Post a Comment