Maafisa wa magereza wakifuatilia mashauri kwa njia Mahakama Mtandao (kushoto) Musa Kaswaka na (kulia) kwake ni George Mwambashi yaliyokuwa yakiendeshwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliofika katika ukumbi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mwenendo wa uendeshaji mashauri kwa njia ya Mahakama Mtandao.
Picha ya pamoja ikionyesha washiriki wa zoezi la mahakama mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
**************************************
Na Innocent Kansha na Salum Tawani
Mahakama ya Hakimu .Mkazi Kisutu
iliyopo Jijini Dar es Salaam leo kwa mara ya kwanza imetoa dhamana ya
mahabusu Bw. Abubakari Seguni aliyepo katika Gereza la Keko kwa njia
ya...
Mahakama Mtandao maarufu kama ‘Video Conference’.
Dhamana hiyo imetolewa na Mahakama
hiyo kwa kushirikiana na Gereza la Keko lilipo katika jiji hilo, wakati
ilipokuwa ikieendesha mashauri nane (8) kwa njia ya hiyo ikiwa ni
mwendelezo.
Mtuhumiwa huyo namba tatu ambaye
anakabiliwa na tuhuma ya rushwa na uhujumu uchumi katika shauri namba
43 la mwaka 2017 la jinai, akiwa na wenzake watano dhidi ya Serikali.
Shauri hilo liletwa mahakamani
hapo kwa ajili ya kutajwa, awali Mwendesha Mashtaka Wakili wa
Serikali, Bi. Ester Martin alidai kuwa shauri hilo halijakamilika kwa
sababu upelelezi wake haujakamilika na linasubiri kibali kutoka Ofisi
ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).
Akisoma masharti ya dhamana
mahabusu huyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhe. Augustina Mmbando alieleza
dhamana ya mshitakiwa ipo wazi kwa kuwa na wadhamini wawili watakao weka
ahadi ya shilingi milioni Sitini (ml. 60) na mmoja kati yao lazima awe
mtumishi wa Umma na kwa pamoja wawasilishe mahakamani hati zao za
kusafiria.
Akiahirisha shauri hilo, Mhe. Mmbando alisema litatajwa tena Januari 2, mwaka huu saa tatu (3; 00) kamili asubuhi.
Mashauri mengine saba ya jinai
yaliyosikilizwa kwa njia hiyo, ambayo yako katika hatua ya awali ya
kutajwa yote yalihusu Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kama
inavyoelekeza Sheria Namba Tatu ya mwaka 2016 iliyofanya mabadiliko
ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura namba 200, ambayo upelelezi wake
haujakamilika na mengine yakisubiri kibali kutoka kwa DPP.
Ambapo shauri la kwanza lilikuwa
linamhusu mtuhumiwa Eke Bidi dhidi ya Serikali, watuhumiwa wengine ni
Wolfgang Sylivester, Xiao Shaudan, Hariri Hariri na wenzake, Mohamed
Ismail Sued na wenzake, Ally Anguzuu Sharifu na wenzake, Maarifa Abbas
Nassor na wenzake na Mohamed Mohamed, wakiwemo wenzake watano wote dhidi
ya serikali.
Mashauri hayo yote yatatajwa tena Januari 27, mwaka huu.
Mmoja wa wananchi waliofika
mahakamani hapo kusikiliza shauri la ndugu yake, Bw. Rajabu Bakari mkazi
wa Kongowe alisema teknolojia ya Mahakama Mtandao ni nzuri ila
angependa kumwona ndugu yake uso kwa uso.
Mashauri hayo yenye mahabusu 24
yameendendeshwa mahakamani hapo kupitia gereza hilo kufikia 10, ambapo
mawili yaliendeshwa wiki iliyopita Januari 10, mwaka huu.
Uendeshaji wa mashauri kwa njia
hiyo ni mojawapo ya malengo ya Mahakama ya Tanzania ya kuweza kusikiliza
mashauri kwa wakati na kupunguza gharama za uendeshaji wa
mashauri hayo mfano kuwalipa mashahidi, kuwasafirisha mahabusu,
usalama wa mahabusu , zikiwemo nyingine.
No comments :
Post a Comment