Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwahutubia wahitimu
wa Astashahada, Stashahada na Shahada katika Mahafali ya Tisa ya Taasisi
ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifungua Kusanyiko la
Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru yaliyofanyika
leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema maneno maalum
ya kuwatunuku wa Astashahada, Stashahada na Shahada katika Mahafali ya
Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani
Arusha na jumla ya wahitimu jumla ya wahitimu 918 walitunikiwa vyeti
hivyo.
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa neno kwa wahitimu wa Astashahada,
Stashahada na Shahada katika Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya
Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya
Jamii Tengeru Dkt Bakari George akieleza mafanikio ya Taasisi yake
katika masuala ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati wa
sherehe za Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru
yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Baadhi ya Wahitimu kutoka Taasisi
ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakisiliza hotuba ya Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo
pichani) wakati wa Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya hiyo yaliyofanyika leo
mkoani Arusha.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa
katika picha ya pamoja na waadhiri na wahitimu kutoka Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru mara baada ya kumalizika kwa Mahafali ya Tisa
ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani
Arusha.
Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
********************************************
Na Mwandishi Wetu Arusha
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka
wahitimu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuleta mabadiliko
katika jamii zinazowazunguka kwa kuzihamasisha kutafuta fursa za
maendeleo.
Ameyasema
hayo leo mkoani Arusha wakati akiwatunuku wahitimu wa Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada na
Shahada katika mahafali ya tisa ya Taasisi hiyo.
Amewaambia
wahitimu hao kuwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni watalaam muhimu sana
katika kuhamasisha jamii katika kujiletea maendeleo yao hivyo
wakatumike katika jamii zao kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na taifa.
“Mkatumike
katika jamii zenu mkalete mabadiliko lazima muoneshe kama mnaweza
msibaki mnalalamika fanya jambo linaloonekana fursa zitakuja” alisema
Mhe. Ummy
Waziri Ummy
amewaasa wahitimu hao kuanza kwa kujitolea katika kazi na kuzingatia
maadili katika maeneo watakayokuwa wanafanya kazi au kuisaidia jamii
kwani hakuna njia ya moja kwa moja ya uhakika wa kupata ajira kama
hawatojitolea.
Pia Waziri
Ummy amewataka Wahitimu hao kuonesha utaalam wao katika maisha yao na
maisha ya jamii inayowazunguka katika kutatua changamoto zao na za jamii
zao kwa kuleta mawazo chanja kwa wananjamii ikiwa na jinsi ya kufanya
changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.
Aidha Waziri
Ummy ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii kuongeza nguvu katika
kuhakikisha wanashirikiana na jamii inayowazunguka katika kuwasaidia
kutatua changamoto zinazowakabili na kuazisha miradi mbalimbali ya
maendeleo.
“Tuoneshe
namna gani wataalam wa maendeleo ya jamii tunaweza kusaidia jamii katika
kufikia kipato cha kati na kuwa na Tanzania ya uchumi wa viwanda”
amesema Mhe. Ummy.
Pia Waziri
Ummy aliwataka wahitimu hao waliopata mikopo ya Serikali kuhakikisha
wanarudisha mikopo ili kuwezesha watanzania wengine wanaohitaji elimu
kupata mikopo kama Serikali ilivyowapatia wao mikopo iliyowasaidia
kufikia kuhitimu.
Naye Katibu
Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wahitimu
hao kuitumia elimu walioipata kuwa nyenzo, zana na funguo ya fursa
mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za kimaisha ili kutumia
utaalamu wao kupata majawabu ya changamoto na suluhisho la matatizo
mbalimbali kwa maendeleo yao na jamii zao.
Ameongeza
kuwa Kada ya Maendeleo ya Jamii ni nyenzo muhimu sana katika maendeleo
ya nchi yoyote na Serikali inathamini sana Taaluma ya Maendeleo ya Jamii
kwani imekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza miradi mbalimbali hapa
nchini.
“Msiwe na
hofu wahitimu kwani nyinyi ni watu muhimu katika jamii yetu na elimu
mliyoipata ikawe nyenzo, funguo na fursa ya maendeleo katika nchi yetu”
alisema Dkt. Jingu
Kwa upande
wake Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George
amewasa wahitimu hao kwenda kuleta mabadiliko katika jamii na
kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko na kutengeneza fursa za ajira
kwa wengine.
“Vyeti
mtakavyopata sio njia au mlango wa ajira nikielelezo cha kusoma sasa
mkaitumie kuhamasisha jamii katika kukabiliana na changamoto za maisha”
alisema Dkt. Bakari
Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru katika mahafali ya tisa kwa mwakawa masomo
2018/2019 imewatunuku jumla ya wahitimu 918 wa Astashahada, Stashahada
na Shahada mbalimbali ikiwemo za Maendeleo ya Jamii, jinsia na upangaji
wa miradi.
No comments :
Post a Comment