Hakimu mkazi mfawidhi wa
Mahakama ya wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi akizungumza na wahitimu wa
mafunzo ya awali ya Sheria (Wasaidizi wa kisheria) hawapo pichani.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo
hayo wakimsikiliza kwa makini Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya
wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi.
Baadhi ya wahitimu wa
mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama
ya wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi.

Mkurugenzi wa shirika la PACESHI, Perpetua Magoke akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya sheria kwa wasaidizi wa kisheria kutoka Halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga

Meneja mradi wa kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa wote mjini na Vijijini kutoka shirika la PACESHI, John Shija akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya sheria kwa wasaidizi wa kisheria kutoka Halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya sheria wakiwa
katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama
ya wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi.
Viongozi wakuu wa Shirika la PACESHI wakiongozwa na
mkurugenzi wa Shirika hilo Bi,Perpetua Magoke wakiwa katika picha ya
pamoja na Mgeni Rasmi hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya
Kahama Evodia Kyaruzi .
Na Salvatory Ntandu – Malunde 1 blog
Wahitimu 80 wa mafunzo ya awali
ya sheria kutoka Halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga, wametakiwa
kutojihusisha na vitendo vya rushwa wanapotoa huduma kwa wananchi katika
maeneo wanayoishi ili kutokomeza vitendo vya jinai katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa Desemba
16,2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kahama,
Evodia Kyaruzi wakati akifunga mafunzo ya siku 15 ya wasaidizi wa
kisheria yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Paralegal Aid
Center Shinyanga (PACESHI) yaliyofanyika mjini Kahama.
“Toeni huduma za kisheria kwa
wazee wasiojiweza,watoto na akina mama wajane ambao haki zao zinaonekana
kupokwa na watu wengine ili waweze kupata masaada zaidi kutoka vyombo
vya sheria kama vile Mahakama”,alisema Kyaruzi.
Alisema kwenye jamii kuna
matukio mengi yanajitokeza kama vile ubakaji kwa watoto,vipigo vya akina
mama,migogoro ya Mirathi,na ndoa za watoto za watoto chini ya miaka 18
hivyo ni budi kuhakikisha wanaisadia jamii kuondokana na jinai hizi
kutokana mafunzo ya sheria mbalimbali walizofundishwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
shirika la PACESHI, Perpetua Magoke alisema endapo wasaidizi hao wa
kisheria wakifanya kazi kwa weledi katika jamii wanazotoka itasaidia
kupunguza matukio ya jinai ambayo yanajitokeza mara kwa mara katika mkoa
wa Shinyanga.
“Mmefundishwa sheria mbalimbali
hakikisheni elimu mlioipata inaleta matokeo chanya na tija katika jamii
zenu kwa kuyasaidia makundi ya watu waliosahaulika katika jamii kama
vile wazee na walemavu” ,alisema Magoke.
Kwa upande wake Meneja mradi wa
kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa wote mjini na Vijijini kutoka shirika
la PACESHI, John Shija alisema ili kukidhi mahitaji ya jamii kupata
msaada wa kisheria PACESHI imeamua kutoa mafunzo hayo kwa wasaidizi wa
kisheria 80 kutoka halmashauri za Msalala,Kishapu,Kahama mji,Manispaa ya
Shinyanga,Ushetu na Halmashauri ya Shinyanga.
“Tumewafundisha sheria mama ya
msaada wa kisheria (Legal Aid Act No 1/2017)ili watambue mbinu
mbalimbali za kuwasidia wahitaji ili kupata msaada stahiki wa
kisheria”,alisema Shija.
Esta Enock kutoka halmashauri ya
msalala na Sita Said Mahonja kutoka Manispaa ya Shinyanga walisema
mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwao kwani awali walikuwa hawana
uelewa kuhusiana na sheria ambapo kwa sasa wataweza kuwahudumia wananchi
wengi kwa haraka sana.
Mafunzo hayo ya siku 15 yalianza mjini Kahama Disemba 2 mwaka huu na kuhitimishwa Disemba 16,2019.






No comments :
Post a Comment