
Msaidizi wa Usajili Mkuu Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Lumambo Shiwala

Akina mama wajasiriamali wakiwa katikakongamano hilo lililofanyika mkoani Arusha
********************************
Wafanyabiashara na wajasiriamali
wametakiwa kulinda/kuwa na nembo za bidhaa ili
kuweza kuingia kwenye
soko la ushindani pasipokuwa na changamoto zisizo za lazima.
Akizungumza katika kongamano la
kiuchumi la wanawake wa Mkoa wa Arusha lililofanyika jijini Arusha
Msaidizi wa Usajili Mkuu Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw.Lumambo Shiwala amesema kuwa wafanyabiashara na ambao wanataka
kupata fursa anawahimiza kusajili ili kulinda alamazao za biashara maana
asije akapoteza juhudi zake zote katika kuandaa biashara yake.
“Hata kama unatengeneza sabuni
ama kitu chochote hakikisha utambulisho au nembo umeilinda kisheria na
taasisi inayoshughulikia na kulinda kisheria biashara au nembo ni
BRELA”. Amesema Bw.Shiwala.
Aidha Bw.Shiwala amesema kuwa mahitaji ya kusajili jina la biashara kwa sasa hivi ni kitambulisho chako cha taifa peke yake.
“Mfanyabiashara au mjasiriamali
ambaye atatakiwa kuingia kwenye ushindani atatakiwa kuwa na jina lake
pekee ili kusudi kulitambulisha kwa wateja wake kwahiyo msiingie kwenye
biashara bila kulisajili jina lako maana anaweza kulichukua mtu mwingine
na kulisajili na kuwa mali yake”. Amesema Bw. Shiwala.
No comments :
Post a Comment