Mtume
Paul Toritseju (kushoto) kutoka Nigeria akizungumza wakati akitoa mada
katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata
mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika
iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja, jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkalimani wake,Mwenyeji wa Kongamano hilo,
Mchungaji Dkt.Sako Mayrick.
Mwenyeji wa Kongamano hilo, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick, akisisitiza jambo.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Mafundisho kwa vitendo katika Kongamano hilo.
Mtume Paul Toritseju (kushoto) kutoka Nigeria, akimkabidhi kitabu, Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa.
Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa, akionesha kitabu hicho.
Mwamasishaji wa vijana kufikia mafanikio, Mhandisi Nicholaus Moses akizungumza katika kongamano hilo.
Mmoja wa wachungaji akitoa neno la shukurani katika kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale
VIJANA wametakiwa kuwa na maono makubwa ili wainuke kiuchumi na kuwa na fedha badala ya kulalamikia kuwa maisha ni magumu.
Wito huo
umetolewa na Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria wakati akitoa mada
katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata
mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika
iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja, jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
” Ukitaka
ufanikiwe kwanza kabisa ni lazima uwe na maono na kuyafanyia kazi na si
vinginevyo” alisema Toritseju. Aidha alisema mafanikio yanaanzia
kichwani, ndani ya mtu na si kwa nje au kinachoonekana
Alisema haiwezekani mtu akawa tajiri lakini hafanyi kazi hapo ni lazima watu watalazimika kuuhoji utajiri alionao.
Alisema
vijana wanapaswa kubadilisha mtazamo wa akili zao ili kuyaendea
mafanikio na kuwa tatizo la umaskini linaanzia rohoni kwani mtu
anatakiwa kuwa na nguvu na roho mpya.
Alisema
mpango wa mungu ni vijana kuimarika kiuchumi na kuongeza idadi ya
vijana wengi zaidi kimafanikio. Hakuna kijana aliyemtegemea Mungu na
akawa maskini
Alisema
Afrika tunafikiria zaidi watoto badala ya kuwa na mipango madhubuti ya
kuanzisha biashara katika nyanja mbalimbali kama mawasiliano, utamaduni,
ujenzi wa viwanja, elimu, kuanzisha blog na kuwa na mawazo mapya.
Alisema
changamoto nyingine kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni matumizi ya
mitaala ya elimu ya kizamani ambayo walitumia wazazi wetu iliyopitwa na
wakati na sasa kuna mabadiliko makubwa na mambo mengi ni mapya.
Mwezeshaji
mwingine katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa akilitoa mada
kuhusu kijana kama kiongozi kwa ajili ya mafanikio ni lazima asimamie
misingi iliyopo ili aweze kumiliki uchumi ambayo ni maono, malengo,
kutumikia wengine, kusali, kutomdharau mtu wala kudharauliwa, kanuni za
utunzaji wa fedha, kwenda na muda na kuwa na mauhusiano na watu
mbalinbali.
Alitaja mambo mengine ya kuweza kumfikisha kijana katika mafanikio kuwa ni kuthubutu, jitihada na kufanya kazi kwa nguvu.
Dkt.Mbelwa
alisema mafanikio hayo yatapatikana kwa kuwepo maono, kujua unapoelekea
na kuwepo kwa taarifa na kama hakuna taarifa huwezi kufanya chochote.
Akizungumzia
suala la viongozi alisema hawachaguliwi bali wanaandaliwa na kuwa
pasipo taarifa huwezi kuwa na kiongozi hivyo alihimiza watu wasome sana
vitabu ili kupata maarifa na si kupoteza muda katika mitandao ya kijamii
kama facebook, twitter na mingine.
Mwenyeji
wa Kongamano la Kwanza la vijana, 2019, Mchungaji Dkt. Sako Mayrick
alizungumzia umuhimu wa vijana wa kuwa na maono kwa ajili ya kumiliki
uchumi kwa kusisitiza kuwa hapa duniani hakuna bosi bali tumeumbwa
kutumikia wenginena watu waache uvivu na uzembe.
No comments :
Post a Comment