Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akikata utepe
kuzindua Mpango Mkakati wa shirika la Rafiki SDO wa mwaka 2020/2024
wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa shirika la Rafiki SDO uliofanyika leo
Jumapili Desemba 22,2019 katika ukumbi wa Karena hotel Mjini Shinyanga.
Kulia ni Mkurugenzi wa Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a, Kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Rafiki SDO, Seif Hamad. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizindua Mpango Mkakati wa shirika la Rafiki SDO wa mwaka 2020/2024.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid
Mfaume akimkabidhi Mkurugenzi wa Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a Mpango
Mkakati wa shirika la Rafiki SDO wa mwaka 2020/2024.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume
(katikati) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a na
Meneja Miradi wa Rafiki SDO Eliud Lazaro (kulia),Mjumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi Rafiki SDO Happiness Misael na Mwenyekiti wa Bodi ya
wakurugenzi Rafiki SDO, Seif Hamad wakionesha Mpango Mkakati wa shirika
la Rafiki SDO wa mwaka 2020/2024.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akilipongeza shirika la Rafiki SDO kwa utendaji kazi wake mzuri.
Wadau na wafanyakazi wa shirika la Rafiki wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume.
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa Shirika la Rafiki wa Mwaka 2020/2024.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akipiga
picha ya pamoja na wadau pamoja na wafanyakazi wa shirika la Rafiki
SDO.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akipiga
picha ya pamoja na wadau pamoja na wafanyakazi wa shirika la Rafiki
SDO.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akipiga
picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO waliopatiwa
vyeti vya utendaji kazi mzuri.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika
la Rafiki SDO limezindua Mpango Mkakati wa miaka mitano ‘Strategic Plan
2020/2024’ utakaojikita katika maeneo nane muhimu ikiwemo sekta ya
afya,elimu,maji na usafi wa mazingira,masuala ya jinsia,VVU na
UKIMWI,watoto wanaoishi katika mazingira magumu na uimarishaji wa
shirika hilo.
Uzinduzi
huo umefanyika leo Jumapili Desemba 22,2019 wakati wa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa shirika la Rafiki SDO uliofanyika katika ukumbi wa Karena hotel
Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja wafanyakazi wa shirika na wadau
mbalimbali.
Akizindua
Mpango Mkakati wa Rafiki SDO 2020/2024, Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akimwakilisha Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Albert Msovela alilipongeza shirika hilo kwa jitihada ambazo
limekuwa likizifanya kuwasaidia wananchi.
“Serikali
ya mkoa wa Shinyanga haina mashaka na utendaji kazi wenu. Mnafanya kazi
nzuri, vipaumbele vyenu ni vipaumbele vya serikali,tunawapongeza na
tutaendelea kushirikiana nanyi ili kuhakikisha kuwa Mpango Mkakati huu
mpya unatekelezeka kwa kiwango kinachotakiwa”,alisema Dkt. Mfaume.
“Miradi
yenu imekuwa ikigusa Mipango Mikakati ya kitaifa hususani katika
masuala ya elimu,afya,VVU na UKIMWI,maji na usafi wa mazingira,masuala
ya ukatili wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi pamoja kusaidia
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mfano watoto waliopewa ajira
migodini”,alieleza Dkt. Mfaume.
Mbali
na kuishukuru Rafiki SDO kwa kuwawezesha kiuchumi na kuwaondoa katika
biashara ya ngono baadhi ya wasichana,aliomba shirika hilo na wadau
wengine kuongeza jitihada zaidi kuwafikia baadhi ya wanawake
wanaojihusisha na biashara ya ngono kwani inadhalilisha utu na kuchangia
maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono.
“Rafiki SDO mmekuwa wadau
muhimu katika kuyafikia makundi maalumu ikiwemo wanawake na wasichana
wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili,mmekuwa mkiwafuata na
kuwawezesha kiuchumi ili waachane na biashara hiyo. Naomba katika mpango
mkakati wenu ujao muongeze jitihada kuwafikia watu hawa pamoja na
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi”,alisema Dkt. Mfaume.
Aidha aliwataka wadau wote
kuunganisha nguvu pamoja kupaza sauti kukabiliana na changamoto ya mimba
na ndoa za utoto,malaria na UKIMWI.
Naye Mkurugenzi wa Rafiki SDO
Gelard Ng’ong’a alisema Mpango Mkakati wao wa mwaka 2020/2020
umezingatia mipango mikakati ya serikali ya Tanzania hivyo wanatarajia
kuwa mpango mkakati huo utaleta matokeo chanya katika mikoa
wanakofanyika kazi ikiwemo Shinyanga,Mara na Simiyu.
“Mpango mkakati huu mpya
umesheheni mambo mengi mazuri na yenye tija kwa wananchi kwani
tumejikita kwenye maeneo muhimu ikiwemo elimu,afya,HIV/AIDs,maji na
usafi wa mazingira,Jinsia wanawake na watoto, makundi maalumu na
uboreshaji maisha”,alieleza Ng’ong’a.
Ng’ong’a alitumia fursa hiyo
kuishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapatia katika
kufanikisha miradi mbalimbali na kuomba ushirikiano huo uendelee kuwepo
ili kuwaletea maendeleo wananchi.
“Katika Mpango Mkakati
uliomalizika 2015/2019 wenye lengo la Kuwa na jamii ambayo watoto,vijana
na makundi maalumu yanawezeshwa na kutambua haki zao ,Serikali na wadau
mbalimbali mmekuwa nasi bega kwa bega,naomba ushirikiano huu uendelee
maradufu ili kufanikisha Mpango Mkakati wa mwaka 2020/2024”,alisema Ng’ong’a.
Mkurugenzi huyo aliwapongeza
wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO kwa utendaji kazi wao mzuri ambao
umelifanya shirika hilo lijulikane na kuaminika na kuwaomba kuongeza
jitihada zaidi kufanikisha utekelezaji wa miradi ya shirika.
No comments :
Post a Comment