
Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora Dkt.
Francis Michael akizungumza na Wakuu wa vyuo vya elimu ya juu
waliokutana kujadili namna ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika
vyuo vya elimu ya juu wakati akifunga kikao hicho kilichofanyika jijini
Dodoma.
Picha na Mpiga Picha Wetu
……………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Dkt.
Francis Michael ameziagaiza Menejimenti za Vyuo vya Elimu ya juu
kuhakikisha wanatekeleza
agizo la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alilolitoa wakati akifungua Kampeni
ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia la kuanzisha madawati ya
jinsia katika Vyuo vya hivyo.
Dkt. Francis
ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kikao kilichowakutanisha
Wakuu wa Vyuo vya elimu ya juu kilichojadili namna ya kupambana na
ukatili wa kijinsia katika maeneo ya Vyuo vya elimu ya juu nchini.
Dkt. Francis
ameongeza kuwa tatizo la ukatili wa kijinsia limekuwa likishamiri
katika Vyuo vya elimu ya juu hivyo amezitaka Menejimenti za Vyuo vya
Elimu ya juu na Vyuo Vikuu Vishiriki kuhakikisha wanaweka Mikakati ya
kupambana na vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa upana wake.
Amesema kuwa
Menejimenti ya vyuo ina wajibu wa kuhakikisha vyuo husika vinatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa Kanuni au Sheria na taratibu kwa kuhakikisha
wanazalisha wataalam bora na wenye weledi wa kutosha ili waweze
kulisaidia taifa katika kuleta maendeleo.
“Mkatekeleze
maagizo haya na nitafuatilia kuona utekelezaji wake na mmefikia wapi,
hatuwezi kuvumilia masuala haya hata kidogo yanaharibu picha ya Vyuo
vyetu na taifa” alisema Dkt Francis.
Aidha Dkt.
Francis amewataka wakuu wa Vyuo hao kuhakikisha watumishi wa vyuo hivyo
wanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na Sheria zilizopo kwa kuwa
waadilifu na kuhakikisha wanaepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
dhidi ya wanawake na wanaume ikiwa ni ukatili wa kihisia, kimwili au
ukatili wa kitandao.
Pia Dkt.
Francis amewataka Wakuu wa vyuo hao kuhakikisha wanafunzi wa watumishi
wanatii Sheria na kanuni zilizopo ili kuwezesha Taasisi za Elimu ya juu
nchini kutimiza malengo yake iliyowekewa na iliyojiwekea kwa ufanisi
mkubwa na kuwezesha kuondokana na vitendo vya kikatili na kujenga
mazingira yaliyosalama katika vyuo hivyo.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi
Mkuu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Semu
Mwakyanjala amesema kuwa Taasisi hiyo imejipanga kupambana na tatizo la
vitendo ya ukatili wa kijinsia hasa wa mitandaoni na tayari baadhi wa
watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani kutoka na kufanya vitendo vya
kikatili mitandaoni kwa kuweke picha na maudhui yasiyofaaa na
yanayoumiza watu kihisia.
No comments :
Post a Comment