
Na Alex Sonna
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 4 ya Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na ilianza kufanya kazi Septemba 2006.
Inadhibiti huduma za nishati
(Umeme, Petroli na Gesi asilia) na Maji na Usafi wa Mazingira na
udhibiti wa sekta hizi kwa pamoja unapunguza gharama za udhibiti na
kuwezesha mapato ya tozo ya sekta ya nishati kugharamia sehemu ya
gharama za udhibiti wa sekta ya maji.
Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini iliandaa Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (BPS) wa mafuta nchini.
Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Aprili 2014,ulibaini kuokolewa kwa Sh.Bilioni 121.6 kwa 2012 na 2013.
Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Aprili 2014,ulibaini kuokolewa kwa Sh.Bilioni 121.6 kwa 2012 na 2013.
Akizungumzia mafanikio na
changamoto ya sekta ndogo ya mafuta, katika warsha ya waandishi wa
habari hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany,
anasema kumekuwepo na mafanikio mbalimbali kupitia mfumo huo ikiwemo
kuokolewa kwa kiasi hicho cha fedha.
“Pia kupungua kwa gharama za usafirishaji na
Premium (TZS 81.9 bilioni katika kipindi cha miaka miwili), kupungua kwa gharama za demurrage kwa TZS 25.7 bilioni, kupungua kwa “ocean losses” kwa TZS 14 bilioni baada ya kubadilisha taratibu za uagizaji mafuta kutoka “Cost, Insurance and Freight” na kuwa
“Delivery at Port”,”anasema.
Premium (TZS 81.9 bilioni katika kipindi cha miaka miwili), kupungua kwa gharama za demurrage kwa TZS 25.7 bilioni, kupungua kwa “ocean losses” kwa TZS 14 bilioni baada ya kubadilisha taratibu za uagizaji mafuta kutoka “Cost, Insurance and Freight” na kuwa
“Delivery at Port”,”anasema.
FAIDA YA BPS
Akizungumzia faida nyingine za
uagizaji wa mafuta kwa pamoja kuwa ni kurahisisha upatikanaji wa takwimu
sahihi za ujazo wa mafuta yanayoingizwa nchini.
“Kurahisisha ukokotoaji wa bei za
mafuta kwa mtindo ulio wazi zaidi,kurahisisha udhibiti wa ubora wa
mafuta yanayoingizwa nchini kwa mfumo huu, Mfumo wa BPS utaendelea
kuleta manufaa makubwa kwa nchi, wadau na wananchi kwa ujumla,”anasema.
Kaimu Mkurugenzi huyo anasema ni muhimu ukaendelezwa mfumo huo na taratibu zake zikazingatiwa na wadau wote.
UBORA WA MAFUTA
Mchany anasema uchakachuaji wa mafuta ni changamoto kubwa hapa nchini.
“EWURA imepambana na tatizo hili ambapo uchakachuaji umepungua kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi asilimia 4 sasa,”anasema
“EWURA imepambana na tatizo hili ambapo uchakachuaji umepungua kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi asilimia 4 sasa,”anasema
Aidha, anasema Septemba 2010,
EWURA ilianzisha Program ya kuweka vinasaba kwenye mafuta yanayotumika
nchini ili kudhibiti uchakachuaji na ukwepaji kodi (fuel dumping) na
kuweka mazingira ya ushindani wa haki.
“Utafiti wa UDSM kuhusu matumizi
ya vinasaba kwa mwaka 2010 – 2013 ulibaini ongezeko la mapato ya
Serikali (kodi) kwa TZS 468.50 bilion, Manufaa haya yanaendelea
kupatikana,”anasema

UBORA WA MIUNDOMBINU YA MAFUTA
Anasema EWURA inadhibiti ubora wa miundombinu ya mafuta kwa ili kulinda afya, usalama na mazingira (HSE).
“Kutokana na udhibiti wa EWURA,
maghala na vituo vya mafuta vimeendelea kuwa bora zaidi, pia EWURA
imeandaa masharti nafuu ili kuvutia wawekezaji kwenye maeneo ya
vijijini.”anasema
TAHADHARI MUHIMU MATUMIZI MAFUTA
Anasema kuna tahadhari mbalimbali
za matumizi ya mafuta zinapaswa kuzingatiwa ikiwamo magari ya kubebea
mafuta kutoegeshwa au kulazwa pasipo husika na badala yake yawekwe
sehemu maalumu zilizotengwa.
Mchany anataja tahadhari nyingine
ni kuwa shughuli zote zinazohusu mafuta ya petroli ni lazima zifanyike
kwa umakini na uangalifu mkubwa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Anaeleza kuwa ni muhimu kuzingatia na kufuata Sheria, Kanuni, Viwango vya ubora na masharti ya leseni wakati wote.
“Tahadhari kubwa zinatakiwa
kuchukuliwa katika shughuli za utunzaji, usafirishaji na utumiaji/uuzaji
wa bidhaa za petroli, pamoja na kuhakikisha kuwa maeneo yanayotumika
yameruhusiwa kwa matumizi ya shughuli za
mafuta,”anasema
mafuta,”anasema
Aidha anasema “Miundombinu kama
vile magari ya kubebea bidhaa za petroli, vituo vya mafuta, maghala
makubwa ya kuhifadhia, vijengwe/au kuundwa kwa ubora unaotakiwa na
kuendeshwa kwa kufuata kanuni za kiusalama, kiafya na kimazingira.”
Mchany anafafanua kuwa miundombinu yote inatakiwa kila wakati iwe na vifaa vya Kuzimia moto na viwe vinafanya kazi.
Anasema inabidi wafanyakazi wafundishwe jinsi ya kutumia vifaa hivyo endapo moto unatokea ili kukabiliana nao.
Pia, anasema madhara makubwa yanaweza kusababishwa na mlipuko wa gari linalobeba mafuta.
“Wananchi wasisogelee gari la
mafuta hasa linapopata ajali, magari ya kubebea mafuta yasiegeshwe au
kulazwa pasipohusika- yaegeshwe na kulazwa sehemu maalumu
zilizotengwa,”anasema.
zilizotengwa,”anasema.
Anasisitiza kwa wakati wote vifaa vya kuhifadhia, kubebea na kusafirishia mafuta vikaguliwe na kuwekwa katika viwango bora.
Mbali na hilo anasema lazima
kuweka alama za tahadhari katika maeneo yanayohusika na shughuli za
mafuta mfano usivute sigara, zima injini, zima simu, vaa vifaa vya
usalama uingiapo mahali hapa.
UTOAJI LESENI
Anafafanua kuwa Ewura imetoa
leseni 1,561 za biashara ya mafuta zikiwemo leseni za Biashara ya Mafuta
ya Jumla 66, Biashara ya Mafuta ya Rejareja 1,397 na leseni 19 kwa gesi
ya kupikia na vilainishi vya mitambo ni 56.
VITUO TEMBEZI VYA MAFUTA

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo ya Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo anasema Ewura imeibuka na mkakati mpya wa kuanzisha vituo vya mafuta vinavyotembea (mobile fuel system) kwa kutumia magari maalumu yaliyotengenezwa kwa kazi hiyo.
Anasema mpango huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa mafuta katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya vijijini.
“Nishati ya mafuta inatakiwa
kuuzwa kwa utaratibu unaokubalika na kwa kuwa kujenga visima vikubwa ni
gharama, njia hiyo ni bora na itakuwa ni rahisi kuwafikia wateja walio
wengi,” anasema Kaguo.
Anasema katika maeneo mengi nchini
wafanyabiashara wadogo wamekuwa wakisafirisha na kuuza mafuta kwa njia
ambazo si sahihi na zinazohatarisha usalama wa vyombo vya watumiaji na
maisha yao wenyewe.
Anafafanua kuwa watu wanatakiwa
kufahamu kuwa kusafirisha kuuza mafuta kwa njia zisizo rasmi kwa kutumia
madumu ni kosa kisheria na pia ni hatari kubwa inayoweza kusababisha
majanga kama milipiko ya moto.
‘’Kutokana na ongezeko la vyombo
vya usafiri kama pikipiki, tumeamua kupunguza gharama za kuanzisha vituo
vya uuzaji mafuta ili viweze kujengwa katika maeneo mbalimbali hasa
vijijini ili kuepuka uuzaji mafuta katika vidumu,” anasema.
No comments :
Post a Comment