Mkuu-wa-Chuo-cha-Ustawi-wa-Jamii-Dkt.-Joyce-Nyoni-akifungua-Kongamano-la-Saba-la-Kitaaluma-Jana-Chuoni-hapo
Prof. Wetengere Kitojo
akiwasilisha mada kwa wanataaluma kwenye kongamano la saba la Chuo cha
Ustawi wa jamii jana Chuoni hapo Kijitonyama Dar es Salaam.
Wahitimu na wanafunzi wa Chuo cha
Ustawi wa Jamii wakifuatilia mawasilisho katika kongamano la Saba la
Chuo hicho lilifanyika jana chuoni hapo Kijitonyama Dar es Salaam.
…………….
Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amefungua
Kongamano la saba la kitaaluma ambalo lilijadili mageuzi ya ajenda ya
uchumi wa viwanda na uhitaji wa ushirikishwaji wa karibu wa Jamii katika
mageuzi hayo ili kufanikisha azma hii kubwa ya
nchi.
Ni utamaduni wa vyuo vya elimu ya juu kufanya kongamano la
kitaaluma kabla ya mahafali ya Chuo ambapo kongamano hilo hujumuisha
wahadhiri, wahitimu, na wanafunzi wa chuo kujadili na kuchangia mada
hiyo kwa manufaa ya mabadiliko ya kitaaluma ya chuo na nchi.
Prof. Wetengere Kitojo aliyekuwa mwezeshaji Mkuu wa mada hii
ameainisha masuala muhimu ya kuzitangia ili kuhakikisha vyuo vya elimu
ya juu vinasaidia nchi katika kufanikisha jamii kuwezeshwa kushiriki
katika mageuzi ya uchumi wa viwanda.
Prof. Kitojo amesema kuna haja kubwa kwa sasa kwa vyuo kuangalia
mitaala yake na ufundishwaji wa wanafunzi, ili viweze kumuandaa
mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujiari au kufungua viwanda, pia vyuo kutoa
elimu isiyo rasmi ya viwanda kwa jamii alitaja kama jambo muhimu vyuo
kufanya ilikuwezesha ushiriki wa wananchi katika uchumi wa viwanda.
Aliongeza na kusema hii itatoa nafasi kwa uchumi wa viwanda sio
tu kubadiilisha tarakimu za mapato ya nchi bali pia mabadiliko ya maisha
ya watu wote na jamii kwa ujumla.
“Tunahuitaji mageuzi ya uwekezaji wa viwanda ambapo tutaona soko
la ajira na vibarua kwa watanzania likiongezeka na sio uwekezaji mkubwa
wa fedha nyingi ambao hauna fursa za ajira kwa watu wetu”. alisema
Prof. Kitojo.
Chuo cha Ustawi wa Jamii kinafanya mahafali ya arobaini na tatu
leo katika viwanja vya chuo hicho kijitonyama Dar es Salaam ambapo
kinatarajia kuwatunuku wahitimu takriban 1300 katika ngazi mbali mbali
za elimu.
No comments :
Post a Comment