Kamanda wa Polisi mkoa wa
morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa
akiwaonyesha wanahabari(hawapo pichani ) panga na msumeno alivyokutwa
navyo, bwana Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto
wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp.
********************************
Na farida saidy morogoro
Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro
Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati
ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya
manispaa hiyo
na alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha
kwenye Maji yaliyokuwa wakitiririka kwa kasi kabla ya kushikiliwa na
Polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad
Mutafungwa Askari wake walipokea taarifa toka kwa raia mwema juu ya
uwepo tukio hilo na baada ya kufika eneo la tukio ambapo ni eneo la
chanzo cha maji wakamkuta mtuhumiwa akiwa na Mtoto wake , na katika hali
ya kushangaza wote walikua uchi wa mnyama.
Aidha katika Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno ambapo pia kunadaiwa kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo Mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa Kihonda, ambae nae anasema muwewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo yasiyo eleweka na siku hiyo ya tukio aliaga anaenda kuogelea.

No comments :
Post a Comment