Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene
amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka Taasisi ya
Kumbukumbu ya Sokoine waliofika ofisini kwake lwa lengo la kuutambulisha
Mradi kuimarisha mfumo wa kupanga bajeti na kuhuisha masuala ya
mabadiliko ya tabianchi.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi hiyo Fasal Issa alisema Mradi huo wenye thamani ya sh.
bilioni 2 utatekelezwa katika wilaya za Mpwapwa, Chamwino na Kondoa
mkoani Dodoma.
Alisema kuwa lengo la
mradi huo ni kujengea uwezo wilaya hizo katika kuboresha uhimili wa
mabadiliko ya tabianchi hususan katika sekta ya maji.
No comments :
Post a Comment