
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya
kuzitaka halmshauri zote nchini kutoa taarifa juu ya uchukuaji wa
mikopo kutoka mabenki ya kibiashara.
………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,amezitaka
halmashauri zote nchini kutoa taarifa Ofisini kwake juu ya uchukuaji wa
mikopo kutoka mabenki ya kibiashara.
Agizo hilo Mhe.Jafo amelitoa leo ofisini kwake jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mhe. Jafo amesema kuwa wale wote
waliochukua mikopo na hawajaanza kuitumia wairudishe haraka ipasavyo
kwani Taasisi zote za Serikali zikiwemo mamlaka za Serikali za Mitaa
hazitakiwi kuchukua mikopo kutoka mabenki ya kibiasha.
“Hayo ni maelekezo kutoka katika
walaka wa Barua ya Katibu Mkuu Hazina barua ya tarehe 13 /12/2016 barua
yenye kumbu kumbu namba CBC.155/233/01 kuwa taasisi zote za serikali na
mamlaka za serikali hazipashi kuchukua mkopo kutoka benki za kibiashara”
Amesisitiza Mhe.Jafo
Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa halmashauri yoyote itakayo wasilisha taarfa zisizo sahihi itachukuliwa hatua za kisheria.
“Hivyo wito wangu kwa halmashauri
hizo ni kuwasilisha taarfa sahihi kulingana na mikopo waliyo chukua
kwani udanganyifu wowote utakao bainika kuwa kuna mikopo ya kimashaka
mashaka ambayo haikufuata taratibu sahihi ofisi itachukua hatua mbali
mbali za kisheria” amesema Mhe. Jafo
Hata hivyo Mhe.Jafo amemtaka
Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kusimamia wakurugenzi
wake wote kuhakikisha wanafanya kazi kwa kanuni , sheria na taratibu za
kazi zinavyowataka kufanya kazi ili kufikia malengo yanayotakiwa katika
utendaji wao.
Jafo amesema kuwa baada ya
halmashauri zote kuwasilisha taarfa hizo katika ofisi za TAMISEMI
itafanya tathimini na kutoa maelekezo baada ya kupima taarfa zilizo
wasilishwa.
No comments :
Post a Comment