Friday, November 29, 2019

WANA HABARI MTAKUWA VIBARUA MPAKA LINI- WAZIRI MWAKYEMBE



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari,  lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi. Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari,  lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Pili Mtambalike akichangia mada katika Jukwaa la Waandishi  wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe, akikata utepe kuzindua kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari katika jukwaa la Waandishi wa habari wanawake, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe na Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, wakionyesha nakala ya kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari, kilichozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jukwa la Waandishi wa Habari Wanawake  lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
 Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, akiandika anayoyasikia wakati wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
……………………
Na Judith Mhina -Maelezo
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu  cha Gender and Media  Handbook in Tanzania wakati wa  maadhimisho  ya miaka
miwili ya  Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania  na Maafisa Uhusiano.
Akizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Kibo ndani ya  hoteli i ya Kimataifa ya Hyatt Regence – The Kilimanjaro  leo Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema “Wana habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.
Hebu tujaribu kutekeleza sheria mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo  zimeiga kiila kitu kilichoandikwa kwenye sheria husika ya kimataifa, badala yake wanaleta mada yao pendwa ya jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe. 
Akijibu risala iliyosomwa  na Mwenyekiti wa Mtandao wa  Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public  Relation Networ,. Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa  waandishi wa habari wanawalke wananyanyaswa kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa ni  pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo, kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya kazi  kama waandishi wa kiume na kujikuta wengi wao wakiwa waadhirika wa kunyanyaswa kijinsia.
Waziri mwakyembe aliongeza kwa kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia  masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana na kuwa na vitendea kazi duni katika vyombo vyao vya Habari.  
Ninashangaa waandishi wa Habari ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala kanuni, katika kuimarisha  taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika masilahi madogo yasiyolingana na kazi mnayofanya au hatopata mishahara kabisa .
Akisisitiza jambo hilo Waziri  amesema “Ni agfadhali kuwa na vyombo vya Habari vichache vinavyojali na lulinda masilahi ya Waandishi wa Habari kuliko kuwa na vyombo vingi ambavyo , haviangalii masilahi ya waandishi wa Habari, kuwalipa mishahara stahiki kwa wakati .
Akitoa agizo kwa  kukabiliana na suala la kupiga vita unyanyasaji kijinsia  Waziri Mwakyembe amesema kuwa nimefurahi kwa kuwa mmeonyesha  namba mbili maalum za simu ambazo yeyote atakayenyanyaswa kijinsia azipige ili kupata msaada. Aidha, Wizara yangu  naiagiza kuwa na namba maalum ya simu ambayo mtanipigia mimi moja kwa moja na kuwatangaza wale wote wanaomnyanyasa wanahabari wanawake ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwenye vyumba vya habari.
Akisisitiza agizo hilo amesema dirisha la Waziri lipo wazi kwa kila mtu bila mashariti yeyote na naomba wanahabari walitumie kweli  kweli, mimi nikiwa kama mzazi na kiongozi ni lazima kuhakikisha suala hili linakuwa historia. 
Naye Mwenyekiti  wa Mtandao wa wanahabari wanawake  na maafisa uhusiano Bi Chacha ameongeza kwa kusema kuwa wanawake wana
Katika hizi siku 16 za kupinga ukatili  wa kijinsia katika vyumba vya Habari Mshauri wa masuala ya wanawake wanahabari Bi Pili Mtambalike amesema “Wanahabari wanawake wananyanyaswa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kupewa kazi nyepesi   ikilinganiswha na waandishi wa kiume katika vyombo vya habari kutokana na kutokujiamini  
Aidha , katika vyombo vingi vya Habari utafiti unaonyesha kuwa  wahariri wengi ni wa jinsia ya kiume japo wapo wanawake ambao wanastahili kuwa wahariri  na wanalingana hata kwa taaluma walizonazo ila hawapewi madaraka na hata hawapandishwi madaraja  kama wenzao wa jinsia ya kiume.
Vilevile waandishi wanahabari  wachanga wakike wananyanyaswa kingono  na waliowengi wanafanya kazi kwenye vyombo hivyo  kama correspondence na kulipwa kulingana na stori   ambayo haiwatoshelezi kimaisha. Pia, Lugha wanazotumia wahariri katika vyumba vya habari ni lugha chafu za kudhalilisha na vitisho.
Akiongelea upande wa pili kama ushauri kwa wanahabari wachanga wanawake amesema kuwa  ipo tabia ya wanahabari hawa wa kike wachanga kujiendekeza ili wapate wepesi wa kufanya kazi  bila kuwa wabunifu kujituma na kuhakikisha wanajifunza kila mara ili kukomaa kitaaluma.
Pili Bi Mtambalike amesema kuwa ipo haja ya kuwa na sera ya jinsia  katika vyombo vya Habari na kuhakikisha sera hizo zinatumika . Utafiti uliofanywa katika vyombo 23 vya Habari sita tu ndio vilikuwa na sera inayoeleweka ambayo haitumiki.
Hivyo tunaomba  Jukwaa la Wahariri Tanzania –TEF liangalie namna gani linaweza kuleta usawa wa kijinsia katika  kuwa na idadi sawa ya wahariri kwa kuwa wanawake walio wengi wanaishia katika ngazi ya Wahariri wasaidizi . Akitoa Takwimu amesema asilimia 26  ya wanawake ndio wahariri wasaidizi waliosalia wote ni jinsia ya kiume wakiwemo wahariri wakuu wa jinsia ya kiume.
Pia, unyanyasaji huu wa wanawake unafanyika hata kwenye upande wa vyanzo vya Habari ambavyo kwa wanawake ni asilimia 36 ,a silimia  64 ya vyanzo vya Habari hutokana na wanaume. Hivyo tunaomba hata wanawake wanahabari walione hili na kuhakikisha wanawahoji wanawake wenzao kama chanzo cha Habari badala ya kujikita zaidi kwa wanaume. Amesema Bi Mtambalike.
Naye Mhariri Mtendaji Bakatri Machumu  ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo na kuwasilisha  taarifa yake kupitia video iliyorekodiwa amesema kuwa kutokana na uzoefu wangu katika tasnia ya Habari waandishi wanawake ni wabunifu na wananafasi kubwa ya kuangalia wanawake ambao wako katika jamii na kusaidiana.
Naye Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bibi Hodan  Addou amesema “ Vyombo vya Habari ni kati ya vyombo vyenye nguvu kubwa hivyo vitumike katika kuhakikisha vinaondoa kabisa suala zima la unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia katika  vyomvo vya Habari”.
Pia, ameongeza kwa kusema kuwa ni lazima kuhakikisha wanahabari wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanatumia taaluma yao bila vikwazo ili kuwaletea maendeleo  mtu momoj ammoja na Taifa kwa ujumla.
Akiongelea kauli mbiu ya mwaka katika maadhimisho  ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania  na Maafisa Uhusiano. Unaosema “Changamkia Fursa sasa” Grabbing Opportunity now  Katibu wa Kamati Mtandao  wa Wanahabari Wananawake Tanzania  na Maafisa Uhusiano, Bi Leah Mushi amesema nafasi za mafunzo ambazo hutolewa na wadau mbalimbali wa sekta wa Habari wakiwemo Wanawake wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Shirika la Mitandao ya Habari- Internews
Aidha, kuna fursa nyingi za mafunzo ya Mitandao ya kijamii  na pia wanatoa vitendea kazi kwa waandishi wachanga wake kwa waume ili waweze kujitegemea  katika kufanya kazi zao na kujiendeleza kitaaluma.
Naye Afisa Uhusiano  wa Kituo cha Umoja wa  Mataifa nchini Tanzania Bi Stela Vuzo, amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa wanahabari wachanga wanawake Tanzania kuchangamkia  fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kusimamia taaluma ya Habari na kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na kupata kazi sehemu mbalimbali duniani na kuacha kulalamika  kuhusu masilahi na mishahara midogo.
Haya tunayoyaona  sasa inatokana na mfumo dume ambao tumeuishi kwa miongo kadhaa ambayo adhari zake zinajitokeza ,  hivyo sio kitu cha ajabu katika jamii zetu, na hayatokei kwenye tasnia ya Habari peke yake bali  ni mfumo wa malezi kwenye jamii zetu ambao unatakiwa ukemewa, upigwe vita na uache kubagua mtoto wa kike na yule wa kiume.  Amesema Mhariri Jesse Kwayu.
Iko haja ya Wadau wa Tasnia ya Habari kuongeza kwa pamoja na kuona umuhimu wa sheria , kanuni na taratibu tulizojiwekea ili kuifanya  sekta ya Habari iwe na mfumo madhubuti unaowafaidisha wana taaluma ya Habari kwa jumla.

No comments :

Post a Comment