Monday, November 18, 2019

WADAU WA AFYA WAMETAKIWA KUTAMBUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAPAKUAJI VYOO


Meneja miradi mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira katika upakuaj wa vyoo na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi ya Water Aid leo jijini Dar es Salaam.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kuelekea siku ya Vyoo Duniani wadau mbalimbali wa Afya nchini wametakiwa kutambua changamoto zinazowakabili watu ambao wanajihusisha na uzibuaji wa mitalo mikubwa
pamoja na kutapisha mashimo ya Vyoo.
Katika jiji la Dar es Salaam pekee zaidi yq asimilia 70 ya wakazi wake yapo katika maeneo ambayo si rasmi.
Maeneo hayo sifa zake kunakuwa na changamoto za upatikanaji wa maji safi na Salama, upatikanaji wa huduma za usafi pamoja na huduma za utupaji wa taka maji.
Ameyasema hayo leo Meneja miradi mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak katika kikao cha waandishi wa habari kwenye ofisi za taasisi ya WATER AID jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari Bw. Twaha amesema kuwa inakadiliwa asilimia 10 ya jiji la Dar es Salaam limeunganishwa katika mfumo wa maji taka hivyo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuibuka magonjwa mbalimbali yanayoambukiza.
“Tukizungumzia katika asilimia hizo, asilimia 90 zilizobaki tunatumia aina nyingine za mifumo, moja kwa moja tunatakiwa kufahamu wanaofanya kazi hizo (kutapisha vyoo) ni wale ambao wanaitwa majina mengi kama vyura ama wavamiaji lulu”. Amesema Bw. Twaha.
Aidha Bw. Twaha amesema kuwa katika ripoti ambayo imeandaliwa imezungumzia changamoto hizo kwa mfanya usafi na imesheheni na kudadavua mkanganyiko wanaopitia wafanyakazi katika sekta ya usafi kwenye nchi zinazoendelea.
Vilevile Bw.Twaha amesema kuwa ripoti hii imeandikwa kwa pamoja kwa shirika la kazi Umimwwnguni, Shirika la Water Aid, Benki kuu ya Dunia na Shirika la Afya Duniani, lengo hasa ni kuinua ufahamu juu ya mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi hao wanayapitia.
Pamoja na hayo Bw. Twaha amesema kuwa Wafanyakazi hao mara nyingi hugusa kinyesi cha binadamu pasipokuwa na vifaa vya kujikinga wala vitendea kazi vilivyobora, kitu ambacho kinawaweka kwenye hatari za kupata magonjwa mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira katika upakuaj wa vyoo na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga amesema kuwa biashara hiyo imekuwa kwa kiasi tangu kuanzishwa kwake kwani mpaka sasa katika maeneo mengi hasa wilayani Kigamboni upakuaji holela wa vyoo umepungua kwa kiasi kikubwa.
“Wapakuaji wa kienyeji wakipata kazi mara nyingi wanakuja kwenye kituo, tumefauru kupanua huduma hiyo kwa kufanya matangazo katika vipeperushi lakini pia tunafanya kazi na halmashauri hasa kamati za afya”. Amesema Bw.Milinga.

No comments :

Post a Comment