Nabu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza mbele ya Wajumbe kutoka
mahakamani wakiongozwa na Jaji Mfawidhi Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu
(wakwanza kushoto waliokaa), wakati wa Kikao, lengo ikiwa ni kuona
jinsi taasisi zinazohusika na hukumu kushirikiana kwa pamoja katika
kutenda haki na kuepusha ucheleweshwaji wa kesi.Kikao hicho kimefanyika
mkoani Simiyu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jaji Mfawidhi
Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu akizungumza na Nabu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati),wakati wa kikao cha
kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utolewaji hukumu na ucheleweshwaji
wa kesi mbalimbali.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Kikao hicho kimefanyika mkoani Simiyu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
*****************************
Na Mwandishi Wetu-Simiyu
Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezitaka taasisi
mbalimbali zinazoshughulika na kutoa hukumu na maamuzi kufanya kazi kwa
pamoja ili
kuwaokoa wananchi wanyonge waliopo katika magereza
mbalimbali nchini.
Ameyasema hayo
Mkoani Simiyu wakati wa Kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Wajumbe kutoka mahakamani wakiongozwa na Jaji Mfawidhi
Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu na Wajumbe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka.
Akizungumza
katika kikao hicho Naibu Waziri Masauni alisema kama mihimili muhimu
katika maamuzi ya watanzania wenzetu waliopo magerezani tunatakiwa
kukutana mara kwa mara ili kuweza kuona ni vipi tunaweza kuwatoa wale
wasio na sababu za msingi za kubakia magerezani
“Wote tulipokea
maagizo ya Mheshimiwa Rais baada ya kutembelea gereza Butimba ambapo
alitoa agizo vyombo husika vikutane ili kuweza kusikiliza kero za
mahabusu wanaokaa muda mrefu bila kesi zao kushughulikiwa na hilo
linaenda sambamba na kila chombo husika kutenda haki na kuzingatia
maadili katika kazi zake,mfano kumekua na malalamiko baadhi ya mahakimu
kupokea rushwa au askari wetu kubambikia watu kesi,si jambo nzuri
kumuweka mtu asiye na hatia gerezani,” alisema Masauni.
Akizungumza
katika kikao hicho Jaji Mfawidhi Kanda ya Shinyanga,Gerson Mdemu,
alisema wao kama mahakama wamejipanga kuhakikisha hukumu zinaenda na
sasa wanauleta utaratibu katika mabaraza ya mikoa ili madai mengine
yaanze kushughulikiwa katika ngazi za chini ili kupunguza mzigo na
mrundikano wa kesi
“Nipo na wajumbe
hawa kutoka mahakamani tukitembelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, lengo
kubwa ni kuona ni jinsi gani shughuli za mahakama zinaenda bila kuleta
matatizo yoyote kwa wananchi ikiwepo uharakishaji wa kesi mbalimbali,
zingine zikianzia ngazi ya chini na kumaliziwa katika eneo husika,”
alisema Jaji Mdemu
Naibu Waziri
Masauni yuko ziara katika mkoa wa Simiyu akikagua shughuli mbalimbali za
taasisi zilizopo chini ya wizara yake ambapo alipata nafasi ya kupitia
Vituo mbalimbali vya polisi mkoani hapo na kuongea na mahabusu.
No comments :
Post a Comment